Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 13,2014 SAA 10:16 ALFAJIRI
Arjen Robben amejibu shutuma za Arsene Wenger kwamba mchezaji huyo ni mzuri sana,lakini ni bingwa wa kupiga mbizi "kijiangusha katika eneo la hatari ” kwa kusema kuwa Boss huyo
wa Arsenal, anajifanya kuwa ni kocha mdogo kwa wakati wote.
Wanaume hao wawili wametupiana maneno baada ya Robben kuhusika katika kisa kingine ambacho Wenger alisema
kiliamua mkondo wa mechi ya 16 bora, pale Mholanzi huyo aliposababisha
penalti ambayo ilipelekea kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny kufukuzwa katika
mechi ya kwanza wakiwa London.
Wenger akaenda mbali zaidi baada ya kumtaja Arjen Robben kuwa ni mchezaji mzuri sana wa Bayern Munich,lakini pia ni mpiga
mbizi hodari, baada ya winga huyo kusababisha penalti nyingine tena ya utata dhidi
ya timu yake katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya siku ya Jumanne.
Bayern, ambao walishinda mechi hiyo 2-0, walisonga kwa jumla ya mabao
3-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi hiyo ya marudiano siku ya Jumanne.
"Mimi siku zote husema kama wewe ni meneja mkubwa,pokea mapungufu yako," aliiambia ITV. "Kama wewe umeshinda, kuwa na furaha,furahia. Lakini kama wewe umepoteza mchezo, usianze kulalamika kuhusu mambo yasiyokuwa na maana (ya kijinga).
"kulikuwa na adhabu mbili lakini sitaki kujitetea.kutoka kwa Meneja Mkubwa anatarajia kidogo zaidi kama yeye akifungwa."
Wenger
pia alidai kuwa uamuzi wa kumtoa kwa kadi nyekundu Szczesny ulikuwa ni tofauti kati ya
timu mbili, lakini bosi wa Bayern Pep Guardiola alisisitiza vinginevyo. "Sisi tulishinda na sisi ni bora kuliko Arsenal katika michezo yote, huo ni ukweli," alihitimisha.

0 Comments