Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 11,2014 SAA 09:50 USIKU
Rais wa Inter Milan Erick Thohir amekanusha kufanya mazungumzo juu ya uhamisho wa Javier Hernandez au Fernando
Torres.
Hernandez
ambaye imekuwa na jukumu dogo katika klabu ya Manchester United msimu huu na amekuwa akihusishwa na taarifa za kuondoka katika klabu hiyo ya Old Trafford.
Inter
wametajwa kutoa ofa kwa Mmexico huyo,na kuwa tayari kupereka ofa nzuri ili kumleta pamoja na mchezaji mwenzake wa United Nemanja Vidic msimu ujao,
lakini Thohir anasisitiza kuwa hakuna mipango huo wa kufanya uvamizi mara mbili katika klabu ya Manchester.
Thohir
pia alizitupilia mbali ripoti ya kumuunganisha Torres na Inter katika mpango wa
muda mrefu wa baadaye, ambapo Chelsea inaendelea kuwa chanzo cha uvumi.
"Chicharito
ni mchezaji mzuri lakini sisi hatukuongea na yeye wala na Torres,"
Thohir aliwaambia waandishi wa habari, kabla ya kuhojiwa juu ya hatima
ya Esteban Cambiasso na Walter Samuel ndani ya klabu hiyo.
Cambiasso, 33, na Muargentina mwenzake Samuel, 35, ni miongoni mwa wa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu.
Mkataba wa Rodrigo Palacio umebakisha mwaka kumalizika lakini
mshambuliaji huyo tayari alitangaza kuwa yeye yuko katika mazungumzo kuhusu kutanua mkataba.
"Na mwisho wa msimu sisi tutathmini wachezaji wote na kuamua ambaye ataishi na ambaye ataondoka," alisema Thohir.
"Tuko katika mazungumzo ya kuongeza mkataba na Palacio."

0 Comments