Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 10,2014 SAA 03:00 USIKU
Bayern
Munich hawawezi kuridhika dhidi ya Arsenal katika mechi yao ya pili
ya ligi ya mabingwa barani ulaya katika hatua ya -16
siku ya Jumanne usiku, kocha
Pep Guardiola ameonya.
Wajerumani hao wanajilinda katika uwanja wao wa Allianz Arena kwa mabao 2-0 ambayo waliyapata walipofunga safari mwezi uliopita huko jijini London.
Katika mchezo wa awali timu
zote mbili zilikosa penalti,na wa kwanza kupiga walikuwa ni
Arsenal,baada ya Jerome Boateng kumkwatua hadi chini Mesut Ozil ndani ya
boksi, Mjerumani Ozil akaenda kupiga penalti lakini golikipa Manuel
Neuer akaokoa mkwaju huo.
Na
kipa wa Arsenal Szczesny alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya
kumchezea vibaya Robben katika eneo lake, na kufanya timu hiyo
kumbadili Santi Cazorla kwa golikipa wa akiba Lukasz Fabians ili
kuziba nafasi hiyo.
Penalti ikaamuliwa ipigwe kwa Timu ya Arsenal,lakini mchezaji wa Bayern München David Alaba alikosa penalti hiyo kwa kupiga pembeni.
Mabao ya FC Bayern München yalifungwa na Toni Kroos Dk.54 na Thomas Müller Dk 88.
Kulingana na kwamba, Guardiola anajua Bayern lazima wapate kikombe chochote kwa nafasi yake.
"Kushinda
2-0 jijini London ilikuwa ni matokeo mazuri sana kwetu, lakini
pia ni hatari," alisema Guardiola, ambaye alishinda 6-1 dhidi Wolfsburg na kujitofautisha na Borussia Dortmund kwa pointi 20 kabla ya mapumziko katika ligi ya
Bundesliga.
"Tuna nafasi nzuri sana ya kupita, lakini tutakuwa katika hali ya kuzingatia kimchezo kiukweli". "Tuna weka mawazo yetu katika njia ya kucheza, na kuonesha nini maana ya uwezo".
"Ligi ya Mabingwa ni mchezo mkubwa kwetu, si kama mchezo wa siku hadi siku katika Bundesliga".
"Tutafanya kazi nzuri ."
"Ligi ya Mabingwa ni mchezo mkubwa kwetu, si kama mchezo wa siku hadi siku katika Bundesliga".
"Tutafanya kazi nzuri ."
"Tuna hakikisha tutakuwa na mpira, na kwamba sisi kweli tuta shambulia vizuri na kwenda katika awamu inayofuata," alisema.
"Ni timu bora sana, hivyo sisi tutahakikisha tunamiliki sana."
Guardiola aliongeza: "Sisi tuta hakikisha hawawezi kufunga goli".
"Watu wanadhani '2 -0 kuna nafasi kwa Munich, lakini hilo ni tatizo kubwa kwetu".
"Wao wana (Per) Mertesacker, (Tomas) Rosicky, (Kieran) Gibbs, (Mikel) Arteta na wachezaji wengi wazuri sana".
"Sitaki kumuona Ozil anadhibiti mchezo. Hilo litakuwa tatizo kubwa kwetu".
"Huu si mchezo rahisi. Tuta shambulia, kuonyesha ubora wetu, kutakuwa na fujo pasipokuwa na mpira."
0 Comments