Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 11,2014 SAA 02:26 USIKU
Kikosi cha waliokuwa wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa
nchini Tanzania Young Africans kinatarajiwa kuwasili
kesho alfajiri
jijini Dar es salaam kwa shirika la ndege la Egypt Air kikitokea jijini
Cairo nchini Misri kilipokuwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly na
kutolewa kwa mikwaju ya penati 4-3 mchezo uliofanyika katika Uwanja wa
El Max jijini Alexandria.
Mara baada mchezo huo uliofanyika siku ya jumapili na wenyeji kufuzu
hatua ya 16 kwa mikwaju ya penati, msafara wa viongozi wa Young Africans
pamoja na wachezaji waliwasili jana mchana jijini Cairo na kufikia
katika hoteli ya Marriot iliyopo eneo la Zamalek.
Balozi wa
Tanzania nchini Misri Bw Mohamed Hamza aliandaa chakula cha jioni
kilichojuimsha wachezaji, viongozi, maofisa ubalozi na familia zao,
waandishi wa habari pamoja na baadhi ya watanzania waishio nchini Misri.
Akiongea
kwa niaba ya serikali Balozi Hamza aliwaambia wachezaji wasivunjike
moyo kwani wamepambana kadri ya uwezo wao, timu ilicheza vizuri lakini
mwisho wa siku bahati haikuwa yao hivyo wajipange upya ili mwakani
waweze kufanya vizuri zaidi ya mwaka huu.
Leo asubuhi kikosi cha
Young Africans kilifanya mazoezi katika uwanja wa Al Ahly uliopo makao
makuu ya klabu hiyo eneo la Zamalek kisha mara baada ya mazoezi viongozi
walipata fursa kuongea na viongozi wa Al Ahly wakiwemo makocha ambao
walitoa pongezi kwa wachezaji wa Yanga kwa kiwango walichokionyesha
katika michezo yote miwili.
Uongozi wa Yanga unawashukuru
wapenzi, wanachama, washabiki na wadau wote wa soka waliokuwa pamoja
katika kuiombea timu ya Yanga kufanya vizuri katika mchezo ambao vijana
walitolewa kwa mikwaju ya penati, wasivunjike moyo nguvu zote
zinaelekezwa kwenye Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumamosi dhidi Mtibwa
Suga ya Morogoro lengo la uongozi na wachezaji ni kutwaa Ubingwa wa VPL
kwa msimu wa pili mfululizo.
Chanzo:youngafricans.co.tz

0 Comments