Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 10,2014 SAA 04:16 USIKU
| Mchawi wa miguu Cristiano Ronaldo (kulia) na mchawi Dynamo katika picha zilizowekwa katika ukurasa wa Instagram wa mchawi huyo |
Muingereza ambaye ni msanii wa maigizo ya mazingaombwe, Dynamo hawakuweza kumuonesha uchawi wake Cristiano Ronaldo katika wigo wa Real Madrid mwishoni mwa wiki lakini
alileta furaha kwa baadhi ya watu maalum katika halfa ya siku ya kuzaliwa kwa mshindi huyo wa Ballon
d'O.| Mzaliwa wa eneo la Bradford, mchawi Dynamo na mchezaji wa Real Madrid Pepe (kushoto) |
| Mchawi Dynamo na mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos (kushoto) |
Mshambuliaji huyo wa Madrid, Ronaldo ametimiza miaka 29 na katika sherehe hiyo ya Madrid siku ya Jumapili
iliyofuatana na ushindi mzuri dhidi ya Villarreal, na kuwafanya pia kuwa juu katika msimamo wa La Liga.
| Unataka kumega?: Huyu ni mchawi wa uwanjani kwa kutumia miguu,akizima mishumaa juu ya keki -na ni mchezaji bora wa mpira wa miguu duniani. |
Steven Frayne ambaye amezaliwa 17 Desemba 1982 anajulikana kwa jina lake la kisanii Dynamo,alizaliwa eneo la Bradford huko West Yorkshire nchini England, na aliziweka
picha yeye mwenyewe akiwa na Ronaldo pamoja na wachezaji wenzake Pepe na Sergio Ramos
baada ya sherehe hiyo ya siku ya Jumamosi na kuandika maelezo "sherehe ya Kuzaliwa ya rafiki (kaka)yangu @ Cristiano ndani ya Madrid! usiku wa maajabu!"
Na Ronaldo akajibu kupitia akaunti yake rasmi yaTwitter, alitilia mkazo "Asante, wewe ni wa ajabu."
0 Comments