Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 17,2014 SAA 12:32 JIONI
Manchester City watapambana na Barcelona siku ya Jumanne usiku bila ya Sergio Aguero,kwa sababu ya kutokuwa vizuri kwa
ajili ya mchezo huo wa ligi ya mabingwa raundi ya 16,kocha Manuel Pellegrini alisema siku ya Jumatatu.
Muargentina 25 ambaye ni mfungaji bora wa City - amekuwa nje tangu mwezi uliopita kutokana na tatizo la misuli, lakini alifunga mara sita katika mechi tano za Ligi ya
Mabingwa msimu huu, alipata tatizo hilo baada ya kufunga
bao katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Tottenham Hotspur siku ya Januari 29
na amekosa mechi tatu za mwisho.
Lakini
Manuel Pellegrini alisema kiungo Fernandinho atapatikana katika uwanja wa
Etihad baada ya kukosekana kwa mechi tatu.
Akizungumza
katika mkutano wake wa vyombo vya habari siku moja kabla ya mchezo,
meneja wa City Pellegrini alisema: "Yeye (Aguero) hakuwepo katika mazoezi leo,na hayuko katika orodha ya kikosi chetu,labda tutamuona siku ya Jumamosi kama ataweza kuwa vizuri, lakini labda pia ni
vigumu."
Fernandinho amerudi katika mazoezi baada ya kupona kutokana na tatizo la misuli, na
Pellegrini alisema kuhusu Mbrazil huyo. "Yeye ana nafasi,yuko katika orodha ya
kikosi".
0 Comments