Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI YA MABINGWA:ALICHOKISEMA ROBERTO MANCINI BAADA YA SARE YA GALATASARAY DHIDI YA CHELSEA

  Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 27,2014 SAA 11:10 JIONI
Roberto Mancini ana amini timu yake ya Galatasaray iliweza kuwa na imani na kujiamini kucheza katika kipindi cha pili baada ya
kupambana na kupata sare ya 1-1 na Chelsea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia hii leo.

Fernando Torres aliipatia bao Chelsea mapema katika dakika ya 9 katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Türk Telekom Arena na kumfanya Mancini kulazimika kufanya mabadiliko baada ya dakika 31 tu,na katika kipindi cha pili ndani ya dakika 64 Aurélien Chedjou aliipatia bao la kusawazisha timu ya Galatasaray na kumfanya Mancini kuamini kuwa mabadiliko yameokoa jahazi


Aliwaambia Sky Sports: "Tulikabiliana na mashambulizi matatu au manne na kufunga Katika kipindi cha pili sisi tulicheza vizuri sana".

"Labda katika kipindi cha kwanza tulikwenda na wachezaji wazuri  na walicheza na hofu pengine, lakini nina furaha kwa kipindi cha pili.

"Kila shambulizi tulipoteza wachezaji wanne katika dakika 20 za kwanza na tulikubali kukabiliana na mashambulizi kila wakati, ambayo ni vigumu dhidi ya Chelsea. 

"Tunahitaji kiungo mwingine." 

"Ndiyo,pengine walistahili kushinda goli lingine, Katika kipindi cha pili sisi tulicheza vizuri sana". 

"Lakini nadhani 1-1 ni matokeo mazuri na tuna mchezo mwingine".
 
"tulijiamini sana katika kipindi cha pili. Tuliwaheshimu sana kwa Chelsea katika kipindi cha kwanza"
 

Post a Comment

0 Comments