Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 22,2014 SAA 01:50 USIKU
Meneja
wa Arsenal Arsene Wenger amesema itachukua muda kwa Mesut Ozil kupata
nafuu kutokana na kukata tamaa baada ya
kukosa penalti muhimu katika Ligi ya
Mabingwa.
Gunners
walipigwa 2-0 na Bayern Munich siku ya jumatano katika uwanja wa Emirates lakini hakuweza
kutumia vema nafasi waliyopata ya penalti baada ya kipa Manuel Neuer kuokoa mkwaju wa
Ozil.
Na Wenger alisema siku ya Ijumaa asubuhi katika mkutano wake na vyombo vya habari kuwa Mjerumani huyo bado ilikuwa na huzuni kutokana na kukosa penalti hiyo.
"Ni juu yake sasa?" alisema meneja. " aliomba radhi baada ya mchezo, lakini masaa 48 ni kidogo kupata nafuu juu ya hilo.
"Ni sehemu ya kazi kukabiliana, pamoja na kukata tamaa na kuonyesha kwamba umekubaliana na hilo".
"Sidhani watu watashangaa kuwa amekosa penalti kwa sababu Bayern walikosa penalti pia".
0 Comments