Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 5,2014 SAA 07:40 USIKU
Gareth
Bale amepona tatizo baada ya kuwa majeruhi na anatarajiwa kurudi katika kikosi cha Real Madrid
kwa ajili ya mechi
ya kwanza ya nusu fainali katika Kombe la Mfalme dhidi ya Atletico Madrid siku ya Jumatano.
Winga
wa huyo wa kikosi cha kwanza cha Wales, msimu wake nchini Hispania umekuwa ukivurugwa na
mfululizo wa majeraha madogo baada ya kujiunga kutoka timu yaTottenham
Hotspur kwa uhamisho uliovunja rekord ya dunia na amekosa mechi mbili za mwisho za
Real baada ya kuumia katika La Liga katika mchezo dhidi ya
Granada Januari 25.
"Gareth
Bale atapatikana," alisema kocha Carlo Ancelotti akiwaambia waandishi
wa habari .
"Amejirudi vizuri na ana fanya mazoezi vizuri siku hizi mbili za mwisho na wachezaji
wengine wa timu," aliongeza kocha huyo raia wa Italia, katika msimu wake wa kwanza , baada ya kuchukua nafasi ya Jose Mourinho.
Ancelotti
alisema kuwa mbali na majeraha, sababu nyingine ya Bale ya kutokuwa vizuri kwa haraka kama ilivyotarajiwa wakati wa mazungumzo yao ya muda
mrefu juu ya uhamisho wake, ni kuvurugika kwa maandalizi yake ya kabla ya msimu.

0 Comments