Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 5,2014 SAA 08:23 USIKU
Mkongwe wa Manchester United Ryan Giggs ameunga mkono kuwa Juan Mata anaweza kuwa mchezaji muhimu (mkubwa)wa
muda wote katika klabu ya Ligi Kuu.
Mata ambaye amewasili Old Trafford, imeiwafanya United wanajitahidi kwa kujiamini na kuzinduka walau kidogo msimu huu, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania kusainiwa
kutoka Chelsea kwa ada ambayo ni rekodi ya klabu ya £ 37.1m wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
Giggs
anasisitiza Mata atafanya kitu cha kuifanya Unitedi kuwa katika daraja frani hivi, na
alipoulizwa kama Mata anaweza kuwa mchezaji mkubwa wa United, Giggs aliiambia
MUTV: "Nadhani anaweza kuwa".
"ni wazi ana vipaji. Sitaki kumuweka katika pressure kubwa mno juu yake, lakini sioni kwa nini ishindikane."
Jumamosi
United walifungwa mabao 2-1 na Stoke, ina maana United wamebaki nafasi ya saba katika msimamo,na wana hatihati ya kushiriki katika Ligi ya Mabingwa.
Lakini
Giggs anahisi kumsaini mchezaji mkubwa kama vile Mata kunaweza kuongeza uwezo mkubwa katika kikosi cha David Moyes ', kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25 ambaye tayari ameweka makazi katika timu hiyo.

0 Comments