Ticker

6/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS:TFF, POULSEN WAKUBALIANA KUVUNJA MKATABA

Na.Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 27,2014 SAA 06:40 MCHANA
Kim pousin akizungumza hii leo baada ya Tff kusitishwa rasmi kwa mkataba wake
Shirikisho la mpira Tanzania TFF limekubaliana kwa pamoja na mwalimu wa Mpira Tanzania Kim Pousin Kwamba wasitishe
huduma ya kufundisha Timu ya Taifa ya Tanzania na makubaliano hayo ni ya pamoja,na kusema kuwa  wamekubaliana kwamba itakuwani siri kwa kuachana kwao kwa maana ya (kisheria ya Kimkataba) kati ya Serikali kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo, Kim Pousin    na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Rais wa Tff Jamal Malinzi,amesema kwamba kwa kipindi hiki mwalimu Salum Madabi ambaye ni kaimu mkurugenzi wa ufundi mwenye reseni ya CAF daraja la kwanza, akishirikiana na Hafidh Bandru ambapo amepata kibali kutoka ZDFA kwa ajili ya jukumu la kuendeleza timu ya taifa ambayo inajiandaa na  mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek,na walimu hao wataongoza kikosi hiko cha Taifa Stars kwa mechi moja tu.
Tunaachana kwa amani:Kim Pousin na Rais wa Tff Jamali Malinzi wakipeana mkono mara baada ya mkutano na na waandishi habari hii leo baada ya kusitisha mkataba wa kocha huyo

"Serikali haita husika na kulipia Gharama za kumaliza mkataba na mwalimu Kim Pousin ,kwa hiyo jukumu hili tutalibeba sisi kama Shirikisho lakini pia ninayo furaha kusema kwamba  wapo wadau na wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania ambao wamekubali kuwa sasa ni muda wa mabadiliko, wamejitolea kulipa nusu ya hizi gharama,ila nasisitiza kuwa TFF sio msemaji wa serikali lakini taarifa zote serikali wanazo na imani yetu ni kwamba wataendelea kutuunga mkono kwa kuendelea kumlipa mwalimu mpya atakeye kuja ili maladi malipo ya mwalimu atakaye kuja yasiwe makubwa kuliko mwalimu aliyepita na sisi tunawahakikishia hilo ilo halitatokea "alisema Malinzi.

Aidha malinzi ameongeza kuwa mpaka sasa kuna maombi zaidi ya 20 yaliyotumwa kwa ajili ya kutaka kazi hiyo ya ukocha kwa Tanzania

"Tumeongea na walimu kadhaa kutoka maeneo mbalimbali duniani,lakini niseme jambo moja, tutahakikisha tunampata mwalimu ambaye katika Rekodi yake ya ufundishaji wa mpira wa miguu,awe amewai kuipereka timu ya Afrika katika fainali za AFCO"


Pia Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Rogasian Kaijage akisalimiana na kocha Kim leo baada ya kocha huyo wa kigeni kusitishiwa mkataba wake

Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Wilfred Kidawa (kati kati)ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya benchi la ufundi,amemshukuru Kim kwa kuwa naye katika kipindi chote,na kumtakia kila la Kheri kwa niaba ya benchi la ufundi
Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.



Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.

Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).



Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.

Post a Comment

0 Comments