IMEWEKWA JANUARI 14,2014 SAA 08:31 USIKU
Cristiano Ronaldo Usiku wa jana jijini Zurich ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa FIFA kwa mara
ya pili katika historia yake,ambapo katika tuzo hiyo alikuwa akishindana na nyota wa Barcelona, Lionel Messi na wa Bayern Munich,
Franck Ribery katika kinyang'anyiro cha Ballon d’Or.
Cristiano Ronaldo alipata kura nyingi zaidi ya wapinzani wake Franck Ribéry na Lionel Messi na kuweza kunyakuwa ushindi huo uliokuwa ukitarajiwa na watu wengi.
Ronaldo
kwa mara ya mwisho aliweza kuchukuwa tuzo hiyo ilikuwa ni mwaka 2008 kipindi hiko akicheza katika klabu ya Manchester United alipofanikisha kubeba ubingwa wa Ulaya na Dunia, kabla
ya baadaye kuondoka na kuhamia katika klabu ya Real Madrid.
Ronaldo alijikuta akimwaga chozi mbele ya mtoto wake, ngwiji la soka duniani, Pele pamoja na watu maarufu kibao.
Marafiki toka zamani |
Yote tisa,kumi ni ujumbe aliouandika mchezaji mwezake wa zamani wa Manchester United Rio Frerdinand katika ukurasa wake rasmi wa Facebook kwa kuonyesha kuunga mkono kwa asilimia 100 tuzo hiyo kuchukuliwa na Ronaldo.
0 Comments