Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA JANUARI 24,2014 SAA 12:15 JIONI
Mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
unaanza kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika
miji ya
Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.
Mabingwa
watetezi Yanga watakuwa wageni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam wakati kwenye jiji hilo hilo Uwanja wa Azam Complex
kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka
Morogoro.
Coastal
Union na Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,
huku Kagera Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba.
Raundi
ya 14 ya ligi hiyo itaendelea Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi
mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi kati ya
Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT Ruvu na
Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Viingilio
kwenye mechi ya Ashanti United na Yanga vitakuwa sh. 5,000, sh. 15,000
na sh. 20,000. Viingilio mechi ya Mkwakwani vitakuwa sh. 10,000 kwa sh.
3,000, Uwanja wa Azam Complex sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa
Kaitaba ni sh. 5,000 kwa sh. 3,000.
0 Comments