Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:WATANZANIA WAZIDI KUKIMBIZA KATIKA MICHUANO YA TENNIS

Na.Herman Kihwili. IMEWEKWA JANUARI 15,2014 SAA 07:39 USIKU
Mchuano ya Tennis inayojulikana kama ITF CAT EA Junior Championship 2014 imeendelea kushika kasi katika viwanja vya
Gymkhana jijini Dar es salaam kwa kushuhudia vijana wakitanzania wanaoshiriki hatua ya mmoja mmoja wakiingia katika fainali .
Mmoja wa vijana hao ni Tumaini Martini Meshuko kutoka Tanzania ambaye amefanikiwa kutinga Fainali ya ITF CAT EA Junior Championship 2014 kwa seti(5-7,6-2,6-0) baada ya kumshinda Ernest Habiyambere kutoka Rwanda.
Kikosi cha vijana wakitanzania wakijifua baada ya michezo
Hatua ya pili ya michuano hiyo itaanza baada ya fainali ya hatua ya kwanza ambayo itapigwa leo taree 15 na kumalizika siku ya jumamosi ya tarehe 18 mwaka huu. 
Timu zinazoshiriki
Lengo la kwanza la mashindano haya ni kuweza kujua nchi ipi kwa Afrika mashariki na kati yenye uwezo na kiwango cha juu cha mchezo wa Tennis,na lengo la pili ni kuweza kuwawezesha vijana wa mchezo huu kuweza kupata alama nyingi iwapo watafika fainali au nusu fainali,na alama hizo zinamuwezesha mchezaji kuweza kupata nafasi  kutoka kwa ITF mbayo itamgharamiwa mchezaji kwenda kwenye Camp nchini Burundi ambapo atajifunza mchezo wa Tennis,na wakati huohuo mchezaji atakuwa anasoma shule.

Na endapo watanzania watafanya vizuri katika mashindano haya,yatatupeleka katika mashindano ya Afrika,ambapo hatua ya kwanza itafanyika Nairobi mwezi wa tatu na hatua ya pili itafanyika Morocco. 
 

Post a Comment

0 Comments