Jose Mourinho amesema kuwa anaelewa Manchester United 'hawana furaha' na hatma yao kwa sasa.
Hata hivyo, bosi huyo wa Chelsea pia amesisitiza kuwa hafikirii
nafasi ya kocha David Moyes katika klabu yake kuwa kuna mashaka yoyote.
Kikosi cha Mourinho
Chelsea kitawapokea United katika mchezo wa siku ya Jumapili (Super Sunday) mwishoni mwa wiki
hii, na Chelsea wata kwenda katika changamoto kwa nafasi ya juu.
Na Mourinho amebaini 'habari za ndani ' na kusema kwamba wote hawakuwa vizuri katika uwanja wa Old Trafford.
"Hisia
zangu, kwa miaka ambayo nilikuwa nawasiliana na Sir Alex na baadhi ya
taarifa za ndani, ni kwamba Man United hawana furaha, lakini wao wako shwari,"
alinukuliwa na Daily Mail.
"Wawe na imani na Davidi,wawe na amani na David. Sidhani David kama ana wasiwasi".
"pressure ni kitu ambacho huja kutoka vyombo vya habari ikiwa matokeo yatokuwa si mazuri"
"Jambo muhimu zaidi katika haya yote ni kutokuwa na pressure ambayo inakuja kutoka nje, na kukubali ukweli wa ndani"
"Meneja yuko shwari na wao wanafikiri huyu ni meneja kwa ajili ya miaka miwili,mitatu,minne au mitano."
"Hivyo wote wako pamoja na wanakwenda kujenga tena timu kubwa, Matokeo mabaya yakimalizika"
"Watarudi kufanikiwa, ingawa pengine watachelewa mno
kushinda ligi kwa sababu wao wana pointi nyingi nyuma ya viongoziwa ligi"alimalizia Jose Mourinho
0 Comments