Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 25,2014 SAA 03:53 USIKU
| Mshabiki wa Coastal Union wakifurahia mchezo hii leo.(picha na mtandao wa Coastal Union) |
Mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara,umeendelea hii leo (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne zilizopigwa katika
miji ya Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.
Mabingwa
watetezi Yanga walikuwa wageni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam,ambapo katika
mchezo huo timu ya Yanga imeeibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya timu ya Ashanti.
Yanga ndio walikuwa wa kwanza kushinda kupitia kwa mchezaji wao Didier Kavumbagu katika dakika ya 50,na bao la pili lilifungwa na David Luhende katika dakika ya 79,na bao la kufutia machozi la Ashanti United lilifungwa na Bright Obinnna dakika ya 59.
Na katika Uwanja wa Azam Complex
kulikuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka
Morogoro,mtanange huo ulimalizika kwa wenyeji Azam Fc kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0,bao pekee lililowekwa nyavuni na mshambuliaji Kiple Herman Tchetche.
Coastal
Union na Oljoro JKT waliumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,na mechi hiyo ikaisha kwa sare ya bao 1 kwa 1,bao la Coastal lilifungwa na Yayo Kato dakika ya 7 baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Kenneth Masumbuko baada ya Hamad Juma
kufanya kazi nzuri ya kumdhibiti beki wa Oljoro na kupiga krosi.
| Yusuf Chipo, Kocha wa Coastal Union akiangalia mchezaji wake Danny
Lyanga akifanya vitu vyake katika mechi ya leo uwanja wa Mkwakwani.(Picha na mtandao wa Coastal) |
Dakika ya 87 dakika chache kabla ya mwamuzi wa leo
Israel Nkongo kumaliza kipute, Hamis Saleh wa JKT Oljoro alitumia vema makosa
ya mabeki wa Coastal Union na kupachika bao lililoamsha benchi la timu yake kwa
furaha,na mchezo ukamalizika kwa sare ya bao 1 kwa 1.
Kagera Sugar wao waliwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba,lakini timu kutoka Mbeya bado imeendeleza ubabe kwa kuibuka na ushindi ugenini wa bao 1 kwa 0,bao pekee lililofungwa na Swita Julius
Raundi
ya 14 ya ligi hiyo itaendelea kesho Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi
mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi kati ya
Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT Ruvu na
Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
0 Comments