Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 25,2014 SAA 08:00 USIKU
Everton
wamethibitisha kwamba mshambuliaji wa Ivory Coast Lacina Traore amejiunga na
klabu yao kwa mkopo kutoka Monaco
kwa ajili ya msimu uliosalia.
Traore, mwenye umri wa miaka 23 amefanyiwa vipimo wiki hii,pamoja na tatizo la misuli,lakini klabu wametoa kibali cha kufanya kazi.
Lacina Traore ambaye amepewa jina la “Gentle Giant”, sababu ikiwa ni kuwa mrefu sana wa futi 6 na nchi 8 na inasemekana ni mwanasoka mrefu kuliko wote.
Bosi wa Everton Roberto Martinez alisema mshambuliaji huyo ni mchezaji ambaye ana kasi na ataimudu klabu hiyo.
"Lacina ni mchezaji ambaye Mimi kwa kweli namuhitaji, ni mtu ambaye yuko vizuri katika nafasi ambayo tunahitaji.," Martinez alisema.
"Yeye ni mchezaji mwenye kipaji sana na tayari tumekubaliana hatua chache za gharama za uhamisho karibu £ 30m." alisema.
Traore alijiunga na Monaco kutoka timu Urusi Anzhi Makhachkala mwanzoni mwa mwezi January, lakini klabu hiyo ya Ligue 1 walikuwa na furaha kumruhusu mchezaji huyo kwenda kwenda nje kwa mkopo ili kupata michezo zaidi.
Traore,
ambaye alifunga mabao 12 katika mechi 24 wakati wa msimu wa 2012-2013,na alicheza pamoja na mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o kipindi akiwa Anzhi baada ya
kujiunga akitokea klabu ya Kuban Krasnodar mwezi Juni 2012.
0 Comments