Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 2.2013 SAA 08:14 USIKU
Lionel
Messi ameanza awamu ya pili ya kupona kutokana na kuumia,na kwamba mshambuliaji huyo wa Barcelona,atakuwa nje
hadi mwezi ujao kwa mujibu wa mtaalamu wa tiba ya mwili wakati muargentina huyo akifanya mazoezi siku ya Jumatatu.
Nahodha
huyo wa Argentina, ambaye anasumbuliwa na matatizo ya mguu aliyoyapata katika mchezo wa Barca mwezi
uliopita, pia alionekana akifanya matangazo mafupi ya mpira ya video ,katika kituo cha TYC Sports.
Messi ambaye ni
mshindi mara nne mfululizo wa tuzo za Fifa Ballon d'Or kwa ajili ya
mchezaji wa mwaka wa dunia,atarudi nyumbani kwao Argentina mwishoni mwa wiki na
kukaa hadi Januari 2 kabla ya yeye kurudi Barcelona.
Baada
ya kuisaidia Argentina kupata kufuzu Kombe la Dunia kwa ushindi wa mabao
5-2 dhidi ya Paraguay mwezi Septemba, Messi amekosa mechi zao zote nne , za kufuzu mbili na za kirafiki mbili, kutokana na kuumia.
0 Comments