Simu zikiuzwa kwa mafungu huko nchini china |
WAFANYAKAZI
wawili wa kampuni ya Swissport jijini Dar es Salaam Daudi Mwenga (49)ambaye ni
dereva katika Kampuni hiyo
na Jakson Kituka( 30), mpokea mizigo wamefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya Ilala jana kwa kosa la wizi wa simu zenye thamani ya Mil.
5.2 mali ya mlalamikaji Sued Hamisi Chemchem.
Mbele
ya Hakimu wa Wilaya Janneth Kinyage ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa
Polisi Cecilia Mkonongo kuwa Novemba 11 ,mwaka huu, Uwanja wa Mwalimu Julius
Nyerere ambapo washitakiwa hao kwa pamoja waliiba simu za mkononi ambazo
zilikuwa katika maboksi.
Ilidaiwa
kuwa washitakiwa hao waliiba katoni 20 aina ya M-Horse zenye thamani y
ash.3,477,600,katoni 10 aina ya Nokia 5200 zenye thamani y ash.338,100 ,aina ya
Sharp zenye thamani y ash.740,000 na Sumsung zenye thamani ya Sh.6,441,000
ambazo zote ni mali ya mlalamikaji Chemchem.
Hata
hivyo washitakiwa hao wote kwa pamoja walikana mashitaka hayo na kesi hiyo
itatajwa tena Disemba 19 mwaka huu.
Hapo
awali Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Renatus Chalya
akizungumzia na waandishi wa habari alisema simu hizo walikizamata baada ya
jeshi hilo kuweka mtego katika viwanja hivyo baada ya ndege ya Qatar Airways
kutua uwanjani hapo.
0 Comments