Na.Jackline Mshana ,IMEWEKWA DISSEMBA 3,2013 SAA 09:45 MCHANA
Jackline Mshana akizungumza leo hii |
Bodi
ya Huduma za Maktaba Tanzania (iliyokuwa ikijulikana kama Bodi ya Huduma za
Maktaba
Tanganyika), ni shirika la umma lililopo chini ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi.
Shirika
hili lilianzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 39 ya mwaka 1963 likijulikana kama
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanganyika. Huduma kwa umma zilianza kutolewa rasmi tarehe 01 Aprili, 1964.
Mwaka
1975, sheria ya mwaka 1963 ilirekebishwa ambapo sheria mpya ya Bunge Namba 6 ya
mwaka 1975 iliundwa na kupelekea jina la shirika kubadilika kutoka Bodi ya
Huduma za Maktaba Tanganyika na kuwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania
(BOHUMATA).
Lengo
kuu la kuundwa kwa BOHUMATA lilikuwa kutoa fursa kwa wananchi wote bila ubaguzi
wa aina yoyote kutumia Maktaba za umma ili kujipatia elimu, maarifa, taarifa
mbalimbali zitakazowasaidia katika kujikwamua kutoka katika umaskini na ujinga
na pia kupata burudani na kudumisha utamaduni.
MAJUKUMU YA BODI
Majukumu
ya msingi ya Bodi yanatekeleza mahitaji ya sheria ya Bunge Namba 6 ya mwaka
1975. Majukumu hayo ni:
·
Kuanzisha,
kuendesha, kuongoza, kuboresha, kutunza na kuendeleza Maktaba za umma kote
nchini kuanzia ngazi ya Mikoa, Wilaya hadi Tarafa.
·
Kuupatia umma wa
Watanzania taarifa mbalimbali zilizokusanywa kutoka katika ulimwengu mpana wa
maarifa kwa ajili ya elimu, utafiti na maendeleo ya kijamii, kiuchumi na
kiutamaduni.
·
Kukusanya na
kuhifadhi machapisho ya kitaifa.
·
Kutoa mafunzo na
kuendesha mitihani ya taaluma ya Ukutubi kwa wafanyakazi wa Bodi, Maktaba za
shule, Vyuo na Taasisi mbalimbali nchini.
·
Kutoa ushauri na
uelekezi kwa Idara za Serikali, Taasisi na Mashirika mengine kuhusu kuanzisha,
kuendeleza na kuboresha huduma za Maktaba katika maeneo yao.
·
Kuendeleza mfumo wa
ushirikiano kati ya Maktaba za BOHUMATA na Taasisi nyingine zinazotunza nyaraka
ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa kwa urahisi.
MTANDAO WA HUDUMA
Bodi
ya Huduma za Maktaba Tanzania inatoa huduma katika mikoa 22, wilaya 19 na
tarafa 2, kutoka Maktaba 3 zilizokuwepo wakati ilipoanza kutoa huduma kwa umma
mwaka 1964.
Dira ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ni kuwa
Taasisi ya umma inayoongoza nchini katika kutoa na kusambaza taarifa mbalimbali
kwa njia ya vitabu, machapisho na teknolojia ya kisasa kupitia mtandao wa
maktaba zake kote nchini.
Dhima ya BOHUMATA ni kutoa na kusambaza huduma
sahihi kwa watu wote kwa wakati muafaka ili kuendeleza kisomo, kujiburudisha na
kuendeleza utamaduni kwa jamii. Pia kukusanya, kutayarisha na kuhifadhi
machapisho kwa matumizi ya kizazi kijacho.
MAFANIKIO
KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2012/2013
1). Bodi
ya Huduma za Maktaba Tanzania iliwezesha kupatikana kwa jumla ya vitabu 25,516;
kati ya hivyo, 468 vilipatikana kwa mujibu wa sheria Na. 6 ya Mwaka 1975,
vitabu 24,984 vilipatikana kwa njia ya msaada na vitabu 64 vilinunuliwa na
hivyo kufanya idadi ya vitabu vyote katika Maktaba nchini kufikia 1,210,473.
2). Ilitoa
ushauri kuhusu uanzishwaji na uendeshaji wa Maktaba katika shule 22 na taasisi
7.
3). Ilipokea jumla ya watumiaji wa Maktaba
1,199,243 ambapo kati yao 999,243 walikuwa wa
muda mfupi na 200,000 wa muda
mrefu.
4). Ilianzisha
miradi miwili yenye lengo la kuipatia jamii habari kwa kutumia TEHAMA kwa
kushirikiana na Chama cha Ukutubi cha Ufini (Finnish Library Association) na
Taasisi ya Electronic Information for Public Libraries ya nchini Ujerumani)
ambapo makundi yafuatayo yalinufaika: wakulima, wafugaji, vijana na
wajasiriamali.
5). Iliwezesha
udahili wa wanafunzi 1,196 wa Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS),
Bagamoyo; ambapo ngazi ya Cheti walikuwa 502, Stashahada 545 na wa mafunzo ya
muda mfupi 149.
6). Ilikamilisha
awamu ya kwanza ya ujenzi wa hosteli kwa ajili ya
wanafunzi wa kike, yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 64 katika Chuo cha Ukutubi
na Uhifadhi Nyaraka (SLADS), Bagamoyo.
7). Ilifanya mkutano mkubwa ujulikanao
kama Maktaba kwa Maendeleo uliokuwa na lengo la kutambua / kuhamasisha jamii
juu ya umuhimu wa Maktaba katika Jamii, ambao ulikutanisha zaidi ya wadau 300
kutoka Tanzania, Kenya, Namibia, Ujerumani, Ufini, na Uingereza.
CHANGAMOTO
Uhaba wa fedha za maendeleo na za matumizi
mengineyo ambao unapunguza kasi ya: kuendeleza na kukarabati miundo mbinu ya
Maktaba, ununuzi wa vitabu, ununuzi wa vifaa vya TEHAMA, uendelezaji wa Chuo
cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS), Bagamoyo na kuwaendeleza watumishi
kielimu.
BOHUMATA imekuwa ikifanya yafuatayo ili
kukabiliana na changamoto hizo:
1). Kuandaa maandiko mradi mbalimbali ya kuombea misaada kwa wafadhili.
2). Kushirikiana
na Halmashauri za wilaya kuendeleza huduma za Maktaba wilayani.
3). Kuendeleza ushirikiano na mashirika mbalimbali
kama vile ‘Book Aid International’ la nchini Uingereza na ‘Children
International’ la nchini Marekani, UNESCO - Tanzania wanaoipatia BOHUMATA
misaada ya vitabu na vifaa vya TEHAMA.
4). Kuwajengea uwezo watumishi wa vituo vya Bodi
ili waweze kutafuta wafadhili wa kuviendeleza vituo hivyo.
MIPANGO IJAYO
1). BOHUMATA
ina mpango wa kuboresha zaidi huduma za Maktaba kwa jamii kwa kutumia TEHAMA
kwa kutumia Katalogi ya Kielektroniki. Hatua iliyofikiwa mpaka sasa ni
kununuliwa kwa ‘server’ na vifaa vingine husika, kuanza programu ya mafunzo kwa
watumishi na inakadiriwa kuwa mpaka kufikia mwezi Machi Mwaka 2014 BOHUMATA
itaanza kutumia Katalogi ya Kielektroniki kwa kuanzia Maktaba Kuu ya Taifa –
Dar es Salaam ndiyo itakayohusika na vituo vingine vitafuata.
2). Itakapofika
tarehe 01 Aprili, 2014 BOHUMATA itafanya maadhimisho ya miaka hamsini (50)
tangu ilipoanza kutoa huduma za Maktaba kwa jamii hivyo umma unafahamishwa
kushiriki ambapo baadhi ya mambo yatakayojiri ni pamoja semina/ kongamano,
mahema ya usomaji na kutangaza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha
miaka 50 kwa vyombo vya habari.
HITIMISHO
BOHUMATA inawashukuru wadau mbalimbali kwa
ushirikiano uliopo katika kusaidia kutekeleza malengo yake ikiwemo wizara mama;
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania,
UNESCO – Tanzania, Ubalozi wa China –
nchini Tanzania, Chama cha Ukutubi cha Ufini, na taasisi ya Electronic Information
for Public Libraries (EIFL).
Maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni
yanategemea kupatikana kwa taarifa sahihi na kwa wakati unaofaa. Hivyo Watanzania
wanashauriwa kutumia Maktaba na rasilimali habari zilizopo ili kuwawezesha
kumudu maisha yao kulingana na fani mbalimbali za maisha.
BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
A: TAARIFA YA
KIPEKEE
1). BOHUMATA
kwa msaada wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imefanikiwa kutanua huduma
za Maktaba karibu zaidi na wananchi ambapo imefikisha huduma hizo katika mikoa
22 na wilaya 19. Kwa ngazi ya mikoa mafanikio ni makubwa na katika wilaya
juhudi zilizopo kulingana na Mpango Mkakati wa Shirika wa mwaka 2008/2009 –
2018/2019 ni kushirikiana na Halmashauri za Wilaya nchini ili kuanzisha huduma za
Maktaba wilayani ambapo mafanikio hayo
yamepatikana katika wilaya za Ruangwa, Chunya, Masasi, Mbulu na Ngara.
2). Upanuzi wa Chuo cha Ukutubi na Uhifanyi wa
Nyaraka (SLADS), Bagamoyo ambapo udahili wa wanafunzi umeongozeka kutoka
wanafunzi 100 mwaka 2007 na kufikia wanafunzi 1,093 mwaka 2013. Chuo hiki
kinatoa mchango mkubwa wa upatikanaji wa wakutubi kulingana na ongezeko la
Maktaba katika taasisi mbalimbali nchini.
3).
Kusaidia kuinua kiwango cha elimu kwa
kusambaza vitabu vya msaada kwa shule nchini hasa katika mikoa ya pembezoni na
pia katika taasisi mbalimbali.
3). Kutoa huduma za Maktaba kwa jamii kwa kutumia
TEHAMA kwa kuwafikia wahusika walipo. Kupitia miradi miwili iliyofadhiliwa na Chama cha Ukutubi cha Ufini (Finnish Library Association) na Taasisi
ya Electronic Information for Public Libraries ya nchini Ujerumani) na
kutekelezwa Dar es Salaam na Morogoro ambapo makundi yafuatayo yananufaika:
wakulima, wafugaji, vijana na wajasiriamali.
4). BOHUMATA
ina mpango wa kuboresha zaidi huduma za Maktaba kwa jamii kwa kutumia TEHAMA
kwa kutumia Katalogi ya Kielektroniki. Hatua iliyofikiwa mpaka sasa ni
kununuliwa kwa ‘server’ na vifaa vingine husika, kuanza programu ya mafunzo kwa
watumishi na inakadiriwa kuwa mpaka kufikia mwezi Machi Mwaka 2014 BOHUMATA
itaanza kutumia Katalogi ya Kielektroniki kwa kuanzia Maktaba Kuu ya Taifa –
Dar es Salaam ndiyo itakayohusika na vituo vingine vitafuata hivyo siku za
usoni BOHUMATA itakuwa ya kisasa zaidi. Pia katika Chuo cha Ukutubi ipo maabara
ya kompyuta.
5). Itakapofika
tarehe 01 Aprili, 2014 BOHUMATA itafanya maadhimisho ya miaka hamsini (50)
tangu ilipoanza kutoa huduma za Maktaba kwa jamii hivyo umma unafahamishwa
kushiriki ambapo baadhi ya mambo yatakayojiri ni pamoja semina/ kongamano,
mahema ya usomaji na kutangaza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha
miaka 50 kwa vyombo vya habari.
B: HITIMISHO
v
BOHUMATA inawashukuru wadau mbalimbali kwa ushirikiano uliopo katika
kusaidia kutekeleza malengo yake ikiwemo wizara mama; Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania, UNESCO – Tanzania, Ubalozi wa China – nchini Tanzania, Chama cha
Ukutubi cha Ufini, na taasisi ya Electronic Information for Public Libraries
(EIFL).
v
Maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni yanategemea
kupatikana kwa taarifa sahihi na kwa wakati unaofaa. Hivyo Watanzania
wanashauriwa kutumia Maktaba na rasilimali habari zilizopo ili kuwawezesha
kumudu maisha yao kulingana na fani mbalimbali za maisha.
0 Comments