Nyota wa Barcelona Lionel Messi, hataenda popote katika utawala
wa rais Sandro Rosell kiongozi huyo alitangaza Alhamisi.
wa rais Sandro Rosell kiongozi huyo alitangaza Alhamisi.
"Kwa muda wote nikiwa rais, lolote liwezekanalo au lisilowezekana
litatendwa kuhakikisha Messi anasalia kitako hapa," Rosell alihimiza
katika hafla ya kuwasilisha mkataba wa ushirikiano baina ya Barca na
kampuni kuu ya elektroniki ya Marekani, Intel.
Sandro Rosell |
"Ni vigumu sana, au tuseme haitowezekana, kuwa Messi ataondoka katika timu hapa."
Mshindi huyo mara nne wa tuzo ya Ballon d' Or anauguza jeraha na
anatarajiwa kurudi uwanjani Januari huku kandarasi yake Barcelona
ikidumu hadi 2018 karibu na wakati nyota huyo atakuwa karibu kuadhimisha
miaka 31 tangu kuzaliwa kwake.
Tetesi kuhusu hatima yake zilizuka Jumanne pale makamu wa rais wa
maswala ya kiuchumi wa Barca, Javier Faus, alipofichua hakuna haja ya
kujadilia kandarasi yake upya.
"Kwanini? Kandarasi yake Ilijadiliwa upya miezi sita pekee iliyopita," Faus aliambia kituo cha redio cha Rac1.
Kulingana na duru za Uhispania, Messi ana kipengere cha Euro milioni 250
kwa yeyote anayetamani kumtia huru kutoka katika minyororo ya kandarasi yake na
Barca ingawaje timu zenye uwezo wa kutimiza hayo ni chache mno.
Uvumi kuhusu uwezekano wa mazungumzo mapya baina ya mshambuliaji huyu na klabu chake umezuka kutokana na swala la mishahara.
Mtani wake wa jadi wa Real Madrid, Christiano Ronaldo, alisaini mkataba
mpya wenye dhamani ya Euro milioni 17 kila mwaka kulingana na gazeti la
Marca na kumfanya awe mchezaji kabumbu anayelipwa kiasi kikubwa nchini
hiyo.
Jarida la Forbes linashikilia Messi anatia kibindoni Euro milioni 16 kila mwaka kwa ulinganishi.
0 Comments