IMEWEKWA DISEMBA 4,2013 SAA 12:15 JIONI
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeipa Tanzania mgawo wa tiketi
260 za Fainali za Kombe la Dunia
nchini Brazil.
Watanzania
wanaohitaji tiketi hizo wanatakiwa kutuma maombi TFF kwa maandishi
wakielezea aina ya tiketi na mechi wanazotaka kushuhudia. Hakuna tiketi
zitakazoombwa FIFA bila kuwepo maombi kwa maandishi.
Tiketi
zilizopo kwa Tanzania ni ifuatavyo; kwa hatua ya makundi (ukiondoa
mechi ya ufunguzi), raundi ya 16 bora, robo fainali na mechi ya kutafuta
mshindi wa tatu ni 250.
Kwa
mechi ya ufunguzi, nusu fainali mbili na fainali (mechi namba 1, 61, 52
na 64) ni tiketi kumi tu ndizo zitakazopatikana. Bei za tiketi ziko
katika viwango vitatu tofauti.
Mechi
ya ufunguzi tiketi zake ni dola za Marekani 495, 330 na 220. Hatua ya
makundi (mechi namba 2-48) ni dola 175, 135 na 90. Hatua ya 16 bora
(mechi namba 49-56) ni dola 220, 165 na 110.
Robo
fainali (mechi namba 57-60) ni dola 330, 220 na 165 wakati nusu fainali
(mechi namba 61 na 62) ni dola 660, 440 na 275. Mechi ya mshindi wa
tatu ni dola 330, 220 na 165. Kiingilio kwa fainali kitakuwa dola 990,
660 na 440.
TFF itawasilisha maombi ya tiketi hizo FIFA kuanzia Desemba 8 mwaka huu hadi
Februari 7 mwakani. Idadi ambayo itaombwa FIFA itatokana na Watanzania
waliowasilisha maombi TFF kwa vile zinaweza zisipatikane tiketi zote
hizo zilitengwa kwa Tanzania.
Hivyo tunasisitiza maombi ya tiketi yatakayofanyiwa kazi ni yale ambayo yamewasilishwa TFF kwa maandishi tu.
FIFA YATANGAZA MAKUNDI YA DROO YA KOMBE LA DUNIA
Fifa mnamo Jumanne ilitangaza makundi ambayo yatatumiwa kufanya droo
ya fainali za Kombe la Dunia la mwaka ujao Ijumaa ambapo timu 32
zitawekwa kwenye makundi manane ya raundi ya kwanza ya timu nne kila
kundi.
Kundi 1 ni la timu nane kuu, na moja itawekwa katika kila Kundi A-H.
Makundi yaliyosalia yamepangwa kuambatana na maeneo ambayo timu
zinatoka.
Wenyeji Brazil watapewa nafasi A1 katika droo hiyo na watacheza mechi ya ufunguzi Sao Paulo mnamo Juni 12.
Kumbuka: Droo ndogo ya kabla ya droo kuu itafanywa kuweka moja ya
timu tisa za Ulaya katika Kundi 2. Timu hiyo ya Ulaya kisha itawekwa
dhidi ya moja ya timu nne kutoka Amerika Kusini ili kudumisha usawa wa
maeneo kwenye droo.
Timu nne zilizotoka Amerika Kusini : Brazil, Uruguay, Colombia,
Argentina zitaunda Kundi X la muda. Timu tatu ambazo hazitajipata
zikipewa timu hiyo ya Ulaya katika Kundi 2 zitarejeshwa katika droo kuu.
0 Comments