Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA FEDHA NA TRA WATOA MSIMAMO WAO JUU YA MATUMIZI YA MASHINE ZA KIELETRONIKI(EFD)

Na.Ngonise Kahise,IMEWEKWA NOVEMBA 19.2013 SAA 01:30 USIKU
Kutokana na mgomo unaoendelea wa wafanyabiashara wa Kariakoo naibu waziri wa fedha Mh Sada Salum amefafanua juu ya
utaratibu wa matumizi ya mashine za kieletroniki[EFD] zenye lengo la kumrahisishia mfanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara za kila siku ili kuondoa usumbufu wakati wa ukadiriaji wa kodi
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salam Mh Sada Salum amesema kuwa walengwa wa mashine hizo ni wafanyabiashara wenye mauzo ya million 14 na zaidi wakiwemo:
-Wenye maduka ya vipuri
-Mawakili
-Wenye maduka ya jumla[sub wholesale shops] 
-Migahawa mikubwa
-Wafanyabiashara wakubwa wa mbao
-Maduka ya simu na vipuri vyake
-Baa na vinywaji baridi
-Studio za picha 
-:"Catering services"
-Wauzaji wa pikipiki
-Maduka makubwa ya nguo
-Na biashara zinginezo

(kutoka kushoto)Naibu waziri wa fedha Mh Sada Salum na Mh.Janeth Mbene
Aidha Mamlaka ya mapato Tanzania imewataka wafanyabiashara na wadau mbalimbali kuwa makini na matapeli wanaojifanya watumishi wa TRA ambao hupita madukani kuwasumbua wafanyabiashara kuhusiana na matumizi ya mashine hizo, na endapo watakutana na watu wa aina hiyo ni wajibu wa mwananchi kudai kitambulisho ambacho nyuma huwa na namba ya mwajiri au kutoa taarifa kwa mamlaka husika.
Sanjari na hayo Mh Sada Salum ametoa wito kwa wananchi kudai risiti wanaponunua bidhaa na kuwasihi wafanyabiashara  wakubwa ambao hawataki kulipa kodi kuacha kuwashawishi na kuwachochea wafanyabishara wengine kugoma kutumia mashine na kuwakumbusha kuwa KULIPA KODI STAHIKI NI WAJIBU WA KILA MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments