Ticker

6/recent/ticker-posts

ANGALIA JINSI JAMII NA MICHEZO ILIVYOMBANA MZEE KINESI,ATOA MSIMAMO WA WACHEZAJI WALIOSAJILIWA NA RAGE

Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 19.2013 SAA 2:05 JIONI
Mahojiano yalifanywa kwenye Gari
Kikao cha kamati ya utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika siku ya tarehe 18/11/2013 na kuhudhuliwa na wajumbe wote ambao ni Mzee Joseph Itang'are,Swedy Mkwahi,Zacharia Hanspope,Dan Manembe,Ibrahim Masoud,Francis Waya na Said Pamba,kimeamua kwa kauli moja kumsimamisha Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Mh.Ismail Aden Rage (MB) Uenyekiti wa klabu ya Simba huku suala lake likipelekwa katika mkutano mkuu wa wanachama kwa maamuzi stahiki.

YAFUATAYO NI MAHOJIANO KATI YA JAMII NA MICHEZO NA  MAKAMU MWENYEKITI WA KLABU YA SIMBA MZEE
JOSEPH ITANG'ARE

Jamii na Michezo:Makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Mzee Itang'are,hebu tuambie ni nini ambacho kimetokea mpaka kamati yenu imeamua kumsimamisha mwenyekiti?

Mzee Itang'are:eee! kamati ya utendaji jana imefanya kikao na ilichokuwa ikiangalia ni katiba,na kikao cha kamati ya katiba ambacho mwenyekiti alitamka wazi kwamba mwezi wa 11 kutakuwa na mkutano wa marekebisho ya katiba,na katika mchakato huo tukaona ni vizuri tukae ili tutimize yale ambayo mkutano mkuu ulikuwa umeamua,lakini juzi wakati anasafiri akawa ameamua kwamba mkutano huo haupo na utaitishwa mwakani,sasa swala hilo likawa limeiweka kamati ya utendaji mahali ambapo si pazuri,kwaiyo tukaona ni vizuri tutimize yale tuliyoagizwa na mkutano mkuu kupitia katiba,kwani katiba iliagiza kamati ya utendaji ikusanye maoni alafu ipeleke kwenye mkutano mkuu wa katiba mwezi wa 11,kwaiyo sisi tumepanga kwa kuwa ilikuwa ilikuwa imepangwa tarehe 28,lakini sisi tumeona ni vizuri tukafanya tarehe 1/12/2013.

Jamii na Michezo:aaah! sasa ni sababu gani ya kumsimamisha,nini hasa kilichowasukuma kumsimaisha?

Mzee Itang'are:sababu hasa ni kwamba amekiuka katiba,kuwa mkutano mkuu umeagiza,na katiba ni kwamba kamati ya utendaji ipeleke hayo kwa wakati huo,katika kipindi cha nyuma tumekuwa na mgogoro ya mikutano wanachama wanadai atutekerezi inavyo takiwa, kwaiyo tukaona amna sababu,na mkutano ni wamarekebisho tu amna sabubu ya mkutano.

Jamii na Michezo:Wakati kamati ya utendaji inapokutana yeye ndiye mwenyekti kwa kawaida,alikuwepo katika mkutano au ni ghafla tu mmemtupa nje ya ulingo naye akiwa hayupo katika mazungumzo hayo?
Mzee Itang'are:Ni kwamba anapoondoka anakaimisha,kwaiyo anaposema ni fanye kazi za mwenyekiti ni pamoja na hizo.

Jamii na Michezo:Kwaiyo sasa hivi tunapozungumza mmemuweka pembeni,kwamaana hiyo hayupo hapa nchini?

Mzee Itang'are:Ndio hayupo hapa nchini.

Jamii na Michezo:Na nafasi yake alikuwa anakaimu nani?

Mzee Itang'are:Nakaimu mimi sasa.

Jamii na Michezo:Kwaiyo wewe kaimu,ikionekana umefanya mapinduzi,yaani umempindua bosi wako?

Mzee Itang'are::(Kwa sauti ya unyonge kidogo) hapana sio mapinduzi,sio kwamba tumemuondoa,sisi tumesema tumepeleka katika mkutano mkuu,kwaiyo mjadala utakuwa katika mkutano mkuu.

Jamiina Michezo:Kwa muda mrefu Rage amekuwa katika misuguano na baadhi ya wanachama wa klabu,yaani kumekuwa na maelewano madogo sana,ni nini kimesababisha mkasubiri muda mrefu mpaka imefikia leo hii?

Mzee Itang'are:aaah! unajua kunapofikia katika mabadiliko ya katiba au nyongeza ya katiba ni kitu ambacho kinagusa  katiba ya Simba,kwengine koooote ilikuwa ni mkutano mala katiba aijatendwa,lakini sasa marekebisho ya katiba ni muhimu sana,kwaiyo kamati ya utendaji imeona kwenye marekebisho ya katiba ni vizuri tukawa sahihi kama mkutano mkuu ulivyoagiza,na tutende kama mkutano mkuu wenyewe.

Jamii na Michezo:Na kuna habari kama mmewaondoa makocha, ili likojee?

Mzee Itang'are:hayo ni mapendekezo ya kamati ya ufundi,imeona timu haifanyi vizuri na marekebisho hayo ni ya kawaida karibu kila timu,kwaiyo tumemuweka kocha aliyekuwa anafundisha timu ya Gol mahiya anaitwa Zdravok Logarusic, na kocha Kibadeni tumemuomba aweze kupumzika.

Jamii na Michezo:Mmemuomba apumzike au mmemtimua kazi?

Mzee Itang'are:kutimua wewe ndio unasema hinyo kwamba tumemtimua,lakini kimsingi ni kwamba amesimama,lakini hizi ni kazi,kuna siku wengine wanaweza kumrudisha.

Jamii na Michezo:Mwenyekiti kama akija amkarudisha Kibadeni wake?

Mzee Itang'are:sisi hatuna pingamizi na Mwenyekitu,kama mkutano mkuu utaamua abaki,basi atakuwa ni mwenyekiti wetu,hilo halina ubaya,tulichofanya ni kwamba katiba inasema kama hutendi kilichokuwa katika katiba,basi adhabu ya nidhamu itachukuliwa ili angalau vitu viheshimiwe vile vilivyokuwa katika katiba.

Jamii na Michezo:Ina maana mkutano mkuu utakapo kuja,Rage atarudi katika mamlaka yake,au amekaa pembeni tayari?

Mzee Itang'are:hapana,ni agenda ndio itaamua kwamba atarudi au asirudi.

Jamii na Michezo:Nini hatma ya kocha msaidizi Jamuhuri Khiwelo?

Mzee Itang'are:Unapo muondoa kocha mkuu,ina maana kocha msahidizi hawezi kuwepo,na ilikuwa haiwezekani ukamtoa kocha mkuu ukamuacha kocha msaidizi.

Jamii na Michezo:kwa hiyo huyo kocha mliyemleta anasaidiwa na nani?

Mzee Itang'are:Atasaidiwa na Sureman Matora

Jamii na Michezo:Sasa timu ya vijana atakuwa inafundishwa na nani?

Mzee Itang'are:Matora ni atakuwa kwa muda,ili kuangalia jinsi gani tutajipanga kwa ajili ya Simba B

Jamii na Michezo:Kuna wachezaji wamesajiliwa hivi karibuni tu,na mwenyekiti Rage,hawa nao mnawapokea au mnamwambia mwenyekiti apumzike nao pembeni?

Mzee Itang'are:Wachezaji wale wamesajiliwa na Simba Sport Clabu,na wamesajiliwa sisi sote tukiwepo,na Rage ni mwenyekiti wetu kweli,alituwakilisha na kwa maana hiyo akuna ubaya.

Jamii na Michezo:Daaa! kwaiyo mwenyekiti kasimamishwa,mhh aya Mzee Itang'are,asante sana.

Mzee Itang'are:asente pia na wewe.


UNARUHUSIWA KU SHARE KWA MARAFIKI ZAKO

Post a Comment

0 Comments