Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 13.2013 SAA 08:06 USIKU
Uzinduzi rasmi kwa ajili ya Kombe la CECAFA Senior Challenge
2013 utakuwa ukifanyika siku ya Ijumaa.
2013 utakuwa ukifanyika siku ya Ijumaa.
Hii imethibitishwa na tovuti ya supersport.com kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kamati ya maandalizi ya CECAFA Gerald Chege.
"Uzinduzi utafanyika siku ya Ijumaa.
Ni matumaini yetu kuwa mpango uliozinduliwa wa Soka kwa amani utakwenda vizuri,vilevile mdhamini wetu mkuu bila kubadilishwa tutakwenda vizuri na wengine wenye nia ya kujiunga na mashindano. " alisema
Chege
Chege
"Hii
ni nzuri katika mashindano na itakuwa inatoa nafasi kwa mashabiki wa soka kujua nini cha kutarajia wakati michuano itakapoanza". alifafanua tena Chege
![]() |
| Nicholas Musonye |
Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amebaini kuwa Nairobi na Machakos kutatatumika kwa ajili ya mechi za awali.
"Kwa
ajili ya usimamizi na mipango rahisi, tutakuwa na mechi za awali
Nairobi na Machakos na kisha miji mingine -Kisumu, Mombasa na Mumias itakuwa ni wenyeji wa ya mechi za mtoano."alisema Nicholas Musonye
Nchi
ambazo zimethibitisha kushiriki ni pamoja na: mabingwa Uganda,
Tanzania, Rwanda, Somalia, Sudan, Zanzibar, Eritrea na Zambia, wakati
Burundi inasubiri kama kutakuwa na taarifa kutoka Kenya Football Federation
(FKF).


0 Comments