Ticker

6/recent/ticker-posts

SULUHISHO LA KUWEKA PESA KATIKA VIBUBU LAPATIKANA...story kamili iko hapa..

 Na.Ngonise Kahise,IMEWEKWA NOV. 12,2013 SAA 02:40 USIKU

Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Ghalib Bilal amezindua benki ya maendeleo iliyo chini ya kanisa la kiinjilisti la kirutheli (KKKT) dayosisi ya pwani jijini Dar es salaam,ambapo benki hiyo inalenga kutoa huduma hususani
kwa wananchi wenye kipato cha chini ili kuwakwamua kiuchumi.
Makamu wa Rais Dr. Mohamed Ghalib Bilal,akikata utepe
Akizungumza katika uzinduzi huo Dr.Bilal amebainisha changamoto kuu za kibenki zikiwemo riba kubwa za mikopo hivyo wananchi huogopa kukopa pamoja na uhaba wa benki hivyo kuhifadhi fedha mahali pasipo sahihi.
Mh.Janeth Mbene
Aidha naibu waziri wa fedha Mh.Janeth Mbene ametoa wito kwa wananchi wa mbalimbali kuchangamkia fursa ya kuwekeza na kujipatia mikopo ili kujikwamua kiuchumi na kuwakumbusha kulipa madeni ili kuimarisha shughuli za kibenki.
Askofu mkuu wa kanisa la kilutheri Tanzania Dr.Alex Malasusa akimkabidhi Makamu wa Rais Mh.Dr. Mohamed Ghalib Bilal tuzo yenye nembo ya  benki ya maendeleo
Hata hivyo askofu mkuu wa kanisa la kilutheri Dr.Alex Malasusa amesema kuwa lengo la benki ni kutoa huduma kwa wananchi bila kujali itikadi za kisiasa,kiuchumi na za kidini na kuongeza kwa kutoa rai kwa wananchi na kununua hisa katika benki hiyo.
Sala ya ufunguzi wa hafla
Picha ya pamoja
Baadhi ya wachungaji waliohudhuria uzinduzi huo

Post a Comment

0 Comments