Ticker

6/recent/ticker-posts

ROBIN VAN PERSIE AACHWA KATIKA KIKOSI CHA UHOLANZI

Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 12.2013 SAA 11:56 JIONI

Mshambuliaji wa Manchester United  Robin van Persie atakuwa nje ya kikosi cha Uholanzi kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Japan
na Colombia, baada ya kulalamika juu ya majeraha katika ncha za vidole.
Van Persie ambaye aliongoza katika ushindi wa United wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal katika Ligi ya Uingereza siku ya Jumapili,atakuwa nje baada ya jopo la madaktari wa kiholanzi kuchukuwa uwamuzi wa kumuondoa baada ya mchezaji huyo kulalamika juu ya maumuvu hayo.

Kiungo wa Feyenoord, Jordy Clasie pia atakuwa nje ya kikosi cha Uholanzi siku ya Jumanne baada maumivu ya  mguu wake uliopondeka.
Kocha Louis van Gaal amemuita kiungo wa Norwich Leroy Fer na Davy Proepper wa Eredivisie leader Vitesse Arnhem kama kuziba nafasi hizo.
Proepper ana umri wa miaka 22 yeye ameitwa kwa mara ya kwanza katika mechi hizo za kimataifa.
Mapema, Dirk Kuyt alijiondo kwa sababu ya kuwa majeruhiwa na nafasi yake ikachukuliwa na nahodha wa Ajax Siem de Jong. 
Uholanzi watacheza na Japan Jumamosi  Genk, Ubelgiji, na siku ya Jumanne inayofuata watacheza na Colombia Amsterdam,na hizo timu tatu zote tayari zimefuzu kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil. 

Post a Comment

0 Comments