Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA JUU YA UJIO WA KOMBE LA FIFA LA DUNIA NCHINI

 IMEWEKWA NOVEMBA 4,2013 SAA 01:15 USIKU
Kombe la FIFA la dunia ambalo litashindaniwa katika fainali za soka mwaka 2014 huko nchini Brazil linatarajia kuja nchini
mwishoni mwa mwezi huu likitokea nchini Ghana ikiwa ni sehemu ya ziara ya kombe hilo barani Afrika. Wenyeji wa ziara ya kombe hilo ambalo kabla ya fainali za dunia za mwaka 2014 litatembezwa katika nchi 88 dunaini kote kampuni ya Cocacola nchini wamesema wanaendelea na maandalizi ya ugeni utakaokuja nchini.
 Meneja mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Yebeltal Getachew amesema wamefarijika juu ya ujio wa kombe hilo ambalo litakua linafanya ziara yake nchini kwa mara ya tatu mfululizo. Amesema Tanzania imepata bahati hiyo kutokana na ushirikiano mzuri unaendelea kuonyeshwa kati ya kampuni ya Cocacola dhidi ya shirikisho la soka duniani kote FIFA tangu mwaka 1950. 
 Kwa upande wa meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka ameeleza uataratibu ambao utatumika wakati wa ziara ya kombe hilo litakapokua hapa nchini, kwa kusema mashabiki na wadau wa soka watapata nafasi ya kupiga picha na kombe hilo kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Novemba 30. 
Mkurugenzi wa michezo nchini Leonard Thadeo
Nae mkurugenzi wa michezo nchini Leonard Thadeo amesema ana hakika ujio wa kombe hilo hapa nchini litaongeza chachu kwa
wadau wa soka kuendelea kufanya juhudi za kupanga mikakati ya kufanya vyema katika soka kuanzia ngazi ya vijana. Amesema mbali na changamoto hiyo pia FIFA wamekua wakiitazama Tanzania kama kichocheo cha kuigwa katika hali ya utulivu na amani katika michezo pamoja na kwenye nyanja zingine za kijamii na hivyo wamekua wakitoa kipaumbele kwa kulileta kombe la dunia kwa mara nyingine tena.

Post a Comment

0 Comments