Na.Ngonise Kahise,IMEWEKWA NOVEMBA 13.2013 SAA 02:46 USIKU
Kampuni ya Delima Group of Company imekabizi vifaa vya michezo kwa mashabiki wa timu za Simba na Yanga walizopo
ughaibuni (marekani).
ughaibuni (marekani).
Kampuni ya Delima Group of Company inayomilikiwa na Devis Mosha imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu za mpira ambazo zinaundwa na watanzania ambao wanaishi marekani na ni mashabiki wa Simba na Yanga.
![]() |
| Mwakilishi wa kampuni ya Delima Group of Company (kushoto),ndugu Emmanuel Mzava,akimkabizi vifaa vya michezo,mwakilishi wa mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi marekani Alex Kassuvi(kulia). |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwakilishi wa kampuni ya Delima Group of Company,ndugu Emmanuel Mzava amemkabizi mwakilishi wa mashabiki hao wanaoishi marekani Alex Kassuvi,vikombe viwili pamoja na jezi seti mbili zenye rangi sawa na timu za hapa nchini za Simba na Yanga.
![]() |
| Alex Kassuvi akifafanua jambo baada ya kukabiziwa vifaa vya michezo |
Aidha Emmanuel ameongeza kuwa,lengo la Kampuni ya Delima Group of Company kidhamini timu hizo zinazoundwa na mashabiki wa Simba na Yanga zilizopo ugenini,ni kuweka hamasa ya ushindani ndani na nje ya nchi,na kuongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu.
![]() |
| kutoka kushoto ni Emmanuel Mzava na kulia anayezungumza ni Alex Kassuvi |




0 Comments