Ticker

6/recent/ticker-posts

UHURU MARATHON:NAFASI NYINGINE KWA WATANZANIA KUHAKIKISHA FEDHA ZINABAKI NDANI YA ARDHI YA TANZANIA,NA SIO KUWAACHIA WAGENI

Na.Ngonise Kahise,IMEWEKWA NOVEMBA 14.2013 SAA 07:22 USIKU
Meneja masoko wa TBL,Fimbo Butallah akizungumza na waandishi (hawako pichani)
Kampuni ya TBL kupitika kinyaji chake kisicho na kilevi cha Gland Malt, wametoa kiasi cha shilingi milioni ishirini (20,000,000/-) kwa ajili ya zawadi za washindi wa mbio ndefu za uhuru,maarufu kama uhuru marathon kwa mwaka huu na sehemu ya maandalizi ya shamrashamra  za mbio hizo,zinazotarajiwa kukufanyika Desemba 8 mwaka huu,ambapo zitaanzia na kumalizikia katika viwanja vya
Leaders Clabu jijini Dar es salaam.

Fimbo Butallah ambaye ni Meneja masoko wa TBL,amesema Kampuni hiyo imeona ni busara na muhimu kudhamini mbio hizo za Uhuru marathon kwa kuwa ni mbio pekee nchini zenye lengo la kuhamasisha umoja,mshikamano na amani ya taifa letu.
"mbio hizo ndio nguzo muhimu za maendeleo ya taifa lolote,hivyo TBL kama kampuni inayotengeneza bidhaa hapa nchini tumeona ni muhimu kuungana na watanzania wenzetu wote kuhakikisha kuwa mbio hizi zinafanyika katika hali ya mafanikio makubwa na kuwa za kufana zaidi"alisema Fimbo Butallah

Aidha Butallah ametoa rai kwa makampuni mengine ya ndani na nje ya nchi kujitokeza kuendelea kutoa michango yao ili kufanikisha mbio hizo zenye kubeba dhima ya taifa letu.
"Lakini pia wajitokeze kwa wingi kushiriki mbio hizo kwani zipo katika makundi makuu manne ambayo ni 3km maalum kwa ajili ya viongozi mbalimbali,5km hizi ni mbio za kujifurahisha hazichagui,na pia 21 na 42 km ambazo ni maalum kwa wakimbiaji nguli"alifafanua Meneja masoko wa TBL Fimbo Butallah.
Mratibu wa Uhuru Marathon,Innocent Melleck.akizungumza(katikati) (Waandaaji wanasema kuna wakimbiaji kutoka nchi mbalimbali duniani,na hii fursa ni nzuri kwa wakimbiaji wetu kuweza kujipatia nafasi ya kufanya vyema katika anga za kimataifa lakini pia ni nafasi ya kuonyesha uzalendo wao kwa nchi yao kwa kushiriki mbio hizo)
Naye bwana Innocent Melleck ambaye ni Mratibu wa Uhuru Marathon amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kuweza kushiriki mbio hizo ambazo zina nia kubwa ya kitukimbusha wajibu wetu wa kutunza amani,umoja na mshikamano miongoni mwetu kama walivyoasisi waasisi wa Taifa hili.

"Kwa muda sasa tumesikia na kuona chokochoko za watu wasiolitakia mema Taifa letu kwa kutaka kutuvuruga,sasa huu ni wakati wa kukumbushana kwamba amani iliyopo si ya kuichezea wala kuifanyia majaribio,inatakiwa tuipiganie kwa nguvu zote" alisema Innocent Melleck
 Pia  Innocent Melleck akaongeza kuwa,nafasi ya kudhamini bado ipo kwa makampuni mengine kama wakitaka kudhamini,na kuwataka watu wakumbuke kuwa,bila amani hakuna chochote kinachoweza kuendelea hivyo wote tunatakiwa kuipigania amani kwa nguvu zote.
 Lakini pia akamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kusisitiza na kuunga mkono pamoja na kuleta amani ndani ya taifa hili.


MCHANGANUA WA UDHAMINI NI KAMA IFUATAVYO:

ZAWADI NI SH.13,400,000
 BURUDANI WAKATI WA TAMASHA NI SH.6,6000,000

Post a Comment

0 Comments