Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 23.2013 SAA 11:35 JIONI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi,amemtaka Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Mh.Ismail
Aden Rage kuitisha mkutano mkuu wa wanachama wake ndani ya siku 14 kuanzia leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam,Malinzi amesema kuwa (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini
kuwa mgogoro katika klabu hiyo baada ya kupokea barua mbili,barua ya kwanza ni kutoka kwa kamati ya utendaji ya
Simba ambayo inasema imemsimamisha Mwenyekiti wake,na barua ya pili ni
kutoka kwa mwenyekiti wa Klabu ya Simba Mh.Ismail Aden Rage ikisema kwamba hatambui maagizo hayo ya kusimamishwa.
Uamuzi
wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba
inayosema: “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba,
kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa
zinaheshimiwa na wanachama wake.”
"Mkutano huo uwe na Agenda 1 tu ya
kujadili mgogoro kati ya mwenyekiti wa simba na kamati ya utendaji,na Tff
itatuma mjumbe wake kuangalia nini kinaendelea na baada ya hapo ataleta
riport kuhusiana na mkutano huo"alisema Mlinzi.
TFF
itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa
Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya
kusikilizwa.
0 Comments