Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA NOV. 21,2013 SAA 09:25 ALASIRI
Mechi
ya kirafiki ya kimataifa ya FIFA Date kati ya Tanzania (Taifa Stars) na
Zimbabwe (The Warriors) iliyochezwa juzi
(Novemba 19 mwaka huu) Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 50,980,000 kutokana na watazamaji
7,952.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 7,776,610.17 wakati wa gharama za uchapaji
tiketi ni sh. 3,682,560.
Asilimia
15 ya uwanja sh. 5,928,124, asilimia 20 ya gharama za mechi sh.
7,904,166 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh.
1,976,041.
Asilimia
60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 17,784,373 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 889,219 ambayo
ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
0 Comments