Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 21.2013 SAA 11:43 JIONI
Lionel
Messi amebaini kuwa alikuwa "na furaha sana" baada ya
kumuangalia Cristiano Ronaldo akiisababishia timu yake ya taifa
ya Ureno kwenda kombe la Dunia la FIFA 2014.
ya Ureno kwenda kombe la Dunia la FIFA 2014.
Ureno
ilijikatia tiketi ya kwenda Brazil siku ya Jumanne,
na Ronaldo alifunga mabao yote manne katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya
Sweden.
Messi,
ambaye amechukua tuzo ya kiatu cha dhahabu kwa ulaya 2013 siku ya Jumatano, amesema
kuwa yeye alikuwa na furaha kumuona Mreno huyo akifika fainali na kumpa sifa maalum nyota huyo wa Real Madrid.
"Nilikuwa na furaha sana kwake wakati yeye akifunga mabao hayo," Messi alisema.
"Ni vizuri kuona timu bora inashinda kwenda Brazil, na Cristiano amekuwa na kiwango kikubwa cha ufungaji kwa miaka mingi".
"Mimi
sijui kama huyu Cristiano ni bora kwa sasa, lakini daima yupo, hufunga mabao katika michezo yote na hucheza katika sehemu yake kwa klabu yake
na nchi yake pia, Amekuwa kama kwamba wa miaka mingi."
"Kama ni wakati bora kwake, au kidogo chini ya kwamba kuna ukaribu hakuna utofauti."
Mshambuliaji huyo wa Argentina pia amebaini nia yake ya kushinda Kombe la Dunia, lakini akataja Brazil, Ujerumani na Hispania kama wanaweza wakapata mapema kushinda kombe hilo.
"Hakika, kushinda Kombe la Dunia ni ndoto kwangu mimi , na wachezaji wote wa Argentina," aliongeza.
"Tunahitaji
kuboresha mambo michache , lakini bado kuna muda wa miezi saba hadi
mashindano kuanza, matumaini yangu tunaweza kushinda, Lakini mataifa mengi yanaweza kufanya hivyo".
"Ujerumani ni timu kubwa, imebeba wachezaji wengi vijana wenye nafasi za juu, maalumu kwangu kama Mesut Ozil."
Messi,
ambaye atakosa kwa wiki nane baada ya kupata matatizo ya misuri katika mechi
dhidi ya Real Betis mapema mwezi huu, pia ilionyesha nia yake ya kubakia katika klabu ya Barcelona kwa ajili ya mapumziko ya kazi yake.
Kumekuwa na uvumi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kuwa alikuwa hanafuraha na wafanyakazi wa matibabu wa klabu yake
mwenyewe, na hasa mtaalamu wa tiba maungo Juanjo BRAU,sababu ni juu ya
jeraha lake kwa kuumia mara
kwa mara.
Hata hivyo, Messi alisema: "Nia yangu ni kukaa pamoja na Barcelona kwa ajili ya mema.
"Ninashukuru
kama wanayosema ni ya kweli, nahao watu wananifanya mimi kufanya vizuri,najisikia
fahari kama wanasema mambo kama hayo,Lakini maisha yangu ni pamoja
na Barcelona."
Wakati
huo huo, orodha ya majeruhi wa Barca inazidi kuongezeka baada ya Dani Alves ambaye atakuwa nje kwa siku saba hadi 10.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Brazil amerudi kutoka katika mechi ya kirafiki na timu ya taifa akiuguza kwa kuumia kwa mguu wake wa kulia.
Victor
Valdes na Jordi Alba tayari wamewekwa pembeni na viongozi timu hiyo ya hispania wakati Xavi Hernandez na Fabregas Cesc pia wakiwa na
mashaka kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Granada.
0 Comments