Ticker

6/recent/ticker-posts

TENGA:NAONDOKA KWA FURAHA KWAKUA NIMEACHA MSINGI,LAKINI SINA SHAKA NA WANAOKUJA MADARAKANI

Na.Herman Kihwili pamoja na Boniface Wambura Mgoyo,IMEWEKWA OKTOBA 25,2013 SAA 05:24 JIONI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anayemaliza muda wake, Leodegar Tenga akizungumza na waandishi wa habari hii leo (hawapo pichani)
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anayemaliza muda wake, Leodegar Tenga amesema anafurahi sana kuondoka madarakani kwani anaamini.......
ameacha msingi katika shilikisho na mchezo wa soka kwa ujumla.
Tenga ameyasema hayo hii leo alipokutana na waandishi wa habari kwa mara ya mwisho katika ofisi za shirikisho la mpira jijini Dar es salaam,
"sikuingia madarakani kwa kutaka urais,bali kutengeneza mfumo mzuri wa kuanzia" alisema Tenga.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Tenga kwa makaini katika mkutano wake wa mwisho akiwa madarakani katika ofisi za Tff
Aidha Tenga amesema kuwa,hana shaka hata kidogo na viongozi watakaochaguliwa madarakani,lakini amewataka kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mwanamichezo.
"kipindi cha miaka kadhaa iliyopita mpira umeendeshwa kwa maadili na kafuata kanuni,watakaokuja waendeleze hizo harakati na nawaunga mkono"alisema Tenga.
(Kutoka kushoto)Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)Boniface Wambura Mgoyo,Mwenyekiti wa chama cha soka cha wanawake Bi.Lina Kessy,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anayemaliza muda wake, Leodegar Teng,Katibu mkuu wa TFF Angetile Osea.
Aidha katika hatua nyingine Leodegar Tenga amesema amefurahishwa na jinsi kampeni za uchaguzi zinazokwenda kutoka na ukweli kuwa wagombea wamekuwa wakielezea kile wanachotaka kuufanyia mpira wa miguu.
 Rais Tenga ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) amesema Watanzania wanataka kusikia ajenda za wagombea.

“Ombi langu ni kwamba kampeni zimeanza vizuri, watu wanazungumza hoja zaidi. Ni jukumu la wajumbe kupima na kufanya uamuzi. Kwangu mimi nimejitayarisha kumkabidhi Katiba, Rais mpya wa TFF,” amesema.

Tenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) amesema kazi kubwa iliyofanywa na uongozi wake ni kujenga taasisi (TFF) pamoja na kuweka mifumo (structure) inayoainisha majukumu ya kila mmoja.

“Ajenda yetu wakati tunaingia madarakani mwaka 2005 ilikuwa ni kujenga taasisi. Tayari taasisi ipo, sasa mtazamo uwe kuushughulia mpira wa miguu wenyewe,” amesema.

Mkutano Mkuu wa TFF unafanyika kesho kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF Waterfront, na tayari wajumbe wa mkutano huo ambao pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi siku inayofuata wameshawasili jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi ambaye ni Ofisa Maendeleo wa kanda hii, Magdi Shams El Din ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ni miongoni mwa wageni watakaohudhuria mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments