Meneja
wa Chelsea Jose Mourinho amepigwa faini ya paundi 8,000 baada ya kukiri kuvunja sheria na kufanya mwenendo usiofaa kwa tabia yake katika mchezo wa
Jumamosi wa Ligi Kuu dhidi ya Cardiff City,wamesema FA.
Mourinho alitolewa katika sehemu yake aliyosimama katika uwanja wa Bridge Stamford na mwamuzi Anthony Taylor dakika 20
kutoka mwisho wa ushindi wa 4-1 naye kumpinga mwamuzi katika kile alijua kuwa Cardiff walikuwa na mbinu zakupoteza muda.
"Kama niko katika mchezo na nimelipa tiketi yangu na
kuwa na wasiwasi kwani nikiona kwamba wakati wote mpira uko nje au
kusimamishwa na mpinzani wetu, ilikuwa nikuchelewesha mpira katika
mchezo, ilichukua chini ya sekunde 21.5, " alisema Mourinho wakati huo.
"Hiyo
ni kupoteza fedha,unalipia tiketi yako na kila wakati mchezo unasimama na unasubiri kwa nusu dakika?kama utazidisha kwa idadi ya mara zote ambao
mchezo ulisimamishwa ...na wewe umelipa kwa ajili ya dakika 90 lakini wewe
utaona dakika 55 au 60. "aliongeza Jose Mourinho
FA imesema katika taarifa yake ya siku ya Alhamisi kuwa faini ni adhabu inayolingana na kiwango cha kosa.

0 Comments