IMEWEKWA SEPT. 29,2013 SAA 3:03 USIKU
Ligi kuu Tanzania bara ameendela hii leo 29 Septemba 2012 katika viwanja vitatu tofauti,huku macho na masikio ya watu wengi
yakielekezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam katika mchezo kati ya timu ya Simba na Jkt Ruvu,na matokeo ya mchezo huo Simba imanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0.
Bao la kwanza la Simba lilipatikana katika dakika ya 23 kwa mkwaju wa penarti kupitia kwa mchezaji Amisi Tambe,na penalti hiyo ilipatikana baada ya Jamal Said wa Jkt Ruvu kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Bao la pili la Simba lilipatikana katika dakika ya 49 kupitia kwa Mchezaji Ramadhani Singano.
Katika uwanja wa Sokoine jijini mbeya Kulikuwa na mchezo kati ya timu ya Tanzania Prisons na matajiri wa bongo Azam Fc A.K.A wanarambaramba,na mpaka amchezo unamaalizika timu hizo zilichoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao 1 kwa 1,bao la Tanzania Prisons lilifungwa na Peter Michael katika dakika ya 39 na bao la kusawaziha la Azan Fc lilifungwa na Kipre Tchetche katika dakika ya 49.
Uwanja wa Azam Complex,kulikuwa na mchezo kati ya timu ya Ashanti United na Mtimbwa Sugar,ambapo pia kulishuhudiwa Sare lakini ni ya mabao 2 kwa 2,Paul Maone na Tumba Swedi walifunga mabao ya Ashanti United,huku maboa mawili ya Mtibwa Sugar yakifungwa na Shaaban Kisiga.
1 Comments
UpEndoGOLF offer best Golf Simulator, Kenya cottage Trampoline Park, Cottages & club restaurant in Kenya with Miniature train track, sports Bar and State of the art spa.
ReplyDeleteVisit Now - https://www.upendogolf.com/