Ticker

6/recent/ticker-posts

REAL MADRID 0 ATLETICO MADRID 1:BALE AONJA UCHUNGU WA MECHI YA NYUMBANI AMBAO HAIJAWAI KUTOKEA TANGU MWAKA 1999....maelezo,video,picha na ushahidi wote uko hapa..

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA SEPT. 29,2013 SAA 7:43 USIKU
Gareth Bale kamwe hawezi kusahau derby  hii ya kwanza kwake ambayo Real Madrid walikuwa  nyumbani,lakini  kwa nguvu za
mashabiki Atletico Madrid wameweza   kushinda derby hii katika  ligi kwa mara ya kwanza katika miaka 14 iliyopita.
Kwenye nyavu: Diego Costa akimuahibisha  kipa wa Real Diego López Rodríguez mapema katika kipindi cha kwanza
Shujaa:Costa imeonekana kuwa mwiba katika katika mechi hii  ya Madrid 

Gareth Bale ambaye aliingia akitokea bechi katika dakika ya 45 ameshuhudia historia hiyo ambapo Kwa mara ya mwisho Atletico Madrid kuwapiga Real katika ligi  ilikuwa ni mwaka 1999,kipindi hicho Real ilikuwa ikiongozwa na kocha John Toshack. 
Siku ngumu: Ronaldo Cristiano akikabiliana na Filipe Luis na Arda Turan
Zilitaka kupigwa kavu kavu:Costa  akibishana na Diego Lopez wa
Real Madrid
 
Bale na  Ronaldo wakijadiliana kabla ya kupiga free-kick isiyokuwa na mafanikio

Bao la Atletico Madrid liliwekwa nyavuni na Diego Costa katika dakika  ya 11 lilitosha kabisa  kuondoka na ushindi huo wakiwa ugenini ndani ya uwanja wa Santiago Bernabu.

ANGALIA VDEO YA BAO LA ATLETICO MADRID

Kikosi cha Real Madrid: Lopez, Arbeloa, Ramos, Pepe, Coentrao, Illaramendi, (Modric 45) Di Maria (Bale 45), Isco (Morata 73), Ronaldo, Benzema. 
Akiba wasiotumika: Casillas, Carvajal, Casemiro, Varane
Kadi za njano: Coentrao, Ramos, Pepe, Arbeloa

Kikosi cha Atletico Madrid: Courtois, Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis, Koke, Tiago, Gabi, Arda Turan (Rodriguez 88), Diego Costa (Baptistao 85), Villa (Garcia 87)

Akiba wasiotumika: Aranzubia, Alderweireld, Guilavogui, Oliver.
Kadi za njano: Turan, Koke, Luis, Costa

Goli: Costa 11

Post a Comment

0 Comments