Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA SEPT 29,2013 SAA 11:03 USIKU
Kijana wa familia: Luis Suarez akisherehekea kwa kuonyesha picha ya mke wake na binti yake pamoja na mtoto wake mpya wa kiume Benjamin
Luis Suarez ameanza kwa kishindo katika Ligi Kuu ya Barclays baada ya kufunga mabao mawili kwa Liverpool na kuzidi kuididimiza chini ya msimamo timu ya Sunderland waliokuwa nyumbani katika uwanja wa Stadium of Light.
Suarez akisheherekea bao lake la kwanza tangu kupigwa marufuku kwa mechi kumi
Daniel Sturridge ndiye aliyeanza kushinda kwa bao la mkono
Mchezaji huyo wa kimataifa wa
Urugwai,amerudi uwanjani baada ya kumaliza adhabu nyake ya kusimamishwa mechi 10,
zilihitajika dakika 36 tu kuweza kushinda bao lake la kwanza katika msimu huu baada ya kupasiwa pasi safi na Daniel Sturridge , na kisha akisherehekea kwa kufunua shati lenye ujumbe maalumu kwa familia yake.
Kocha wa muda wa Sunderland Kevin Ball ameonja joto la jiwe kwa kufungwa katika mchezo wake wa kwanza wa ligi
Wacha hapo: Martin Skrtel akikabiliana na mchezaji wa Sunderland Jozy Altidore
Anaongoza: Altidore katika changamoto na Kolo Toure
Mshambuliaji Daniel Sturridge ndiye aliyekuwa wa kwanza kushinda kwa upande wa Liverpool katika dakika ya 28 baada ya kuunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Steven Gerrard na mwamuzi Howard Webb kushindwa kuona
kwamba mpira ulikuwa umegusa na mkono wake, na ndiye yeye pia aliye sababisha bao la tatu lililofungwa na Suarez katika dakika ya majeruhi na kufanya matokeo hadi mwisho wa mchezo kusomeka 3 -1.
Akimaliza mchezo: Suarez akifunga bao la pili katika dakika ya 89
Bao peke la Sunderland waliokuwa nyumbani katika uwanja wa Stadium of Light lilifungwa na Emanuele Giaccherin katika dakika ya 52.
0 Comments