IMEWEKWA SEPT 4,2013 SAA 1:00 USIKU
Mchezaji
mpya wa Real Madrid Gareth Bale hajahakikishiwa moja kwa moja kuwa
atakuwa muda akianza katika kikosi cha kwanza pamoja na yeye kuwa
mchezaji mwenye thamani kubwa kuliko wote baada ya kununuliwa hivi
karibuni na klabu hiyo.
Kocha msaidizi wa Real Madrid Paul Clement amesema kuwa Gareth
Bale licha ya kununuliwa kwa gharama kubwa ya zaidi ya paundi mili0ni
85 haimanishi kuwa kila mara atakua akianza katika kikosi cha kwanza.
Mchezaji mpya wa Real Madrid Gareth Bale hajahakikishiwa moja kwa moja kuwa atakuwa muda akianza katika kikosi cha kwanza pamoja na yeye kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa kuliko wote baada ya kununuliwa hivi karibuni na klabu hiyo.
Paul Clement amesema kuwa ndani ya klabu hiyo kuna ushindani mkubwa
hivyo Gareth Bale pamoja nawachezaji wengine hawawezi wakahakikishiwa
namba kulingana na hali halisi.
Kocha huyo msaidizi amesema kuwa mambo yatakuwa yakibadilika kulingana na mahitaji ya wakati huo na kwa namna kocha mkuu ataona inafaa.
Paul Clement ameongeza kusema kuwa kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti anafahamu namna ambavyo atamtumia mchezaji Gareth Bale lakini si lazima awe na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
CHANZO:rfi Kiswahili

0 Comments