Ticker

6/recent/ticker-posts

BAADA YA KUMKOSA LEIGHTON BAINE,MANCHESTER UNITED WAKWAMA PIA KUMCHUKUWA MCHEZAJI ANAYEKAA BECHI KUTOKA REAL MADRID

Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 3,2013 SAA 8:00 USIKU
Fabio Coentrao amekwama kujiunga na Manchester United kutoka Real Madrid kwa mkopo wa muda mrefu.
United bado kidogo tu kumchukuwa: Fabio Coentra
Mreno  huyo mwenye umri wa miaka 25 ni beki wa kushoto kutoka Real Madrid na amekuwa akikaa bechi bila kucheza katika msimu
huu, kutokana na kushindwa kuleta muonekano mzuri katika ligi,na hiyo ni baada ya kupoteza nafasi kadhaa katika michezo.
United walitaka kumchukua Coentrao baada ya kushindwa katika mpango wa kumchukua mchezaji wa`Everton  Leighton Baine.
Meneja David Moyes aliulinda mpango huu wa kumchukuwa mchezaji huyo kwa saa 11 kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya jumatatu usiku,lakini aliambulia patupu.

Post a Comment

0 Comments