Ticker

6/recent/ticker-posts

VIATU KUTOKA LOS ANGELES MAREKANI,KUPEWA WATOTO WASIOJIWEZA TANZANIA

Na. Herman Kihwili IMEWEKWA AGOSTI 20,2013 SAA 11:25J IONI

Chama cha msalaba mwekundu (Tanzania Red Cross Society) kinazindua Mradi wa ugawaji wa viatu kwa watoto wa shule na wa vituo vya kulelea watoto zaidi ya 500,000 kutoka Mikoa minane ya Tanzania. 
Dr.George Nangale,ambaye ni Rais wa chama cha msalaba mwekundu
Akizungumza na waandishi wa habari Dr.George Nangale,ambaye ni Rais wa chama hiko,amesema Mikoa
itakayonufaika na mradi huu ni pamoja na Shinyanga, Tanga, Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Pwani, Dar-es-Salaam  na Zanzibar na kusema mradi huo utahusisha Watoto wenye umri mdogo wasio jiweza kwani wengi wao  wanaathirika na magonjwa mbalimbali  yanaosababishwa na minyoo.
Detha Mlaya ni mkurugezi wa Idara ya Afya
 Aidha Dr.Nangale ameongeza kuwa, Viatu hivyo aina ya raba nyeusi, ni msaada kutoka kampuni ya Toms Shoes, iliyoko Los Angeles Marekani, unaolenga watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwanunulia aina yoyote ya viatu, na kutoa wito kwa watanzania,kwamba viatu hivyo haviuzwi na havitakiwi kuuzwa kwa watoto au wazazi wa watoto.
Dr.George Nangale akimvalisha viatu mmoja wa watoto waliohudhulia halfa hiyo
Detha Mlaya ambae ni mkurugezi wa Idara ya Afya pia alimvalisha mtoto viatu hinyo
Pia Dr.Nangale amesema  Zaidi  ya voluntia 1,000 kutoka Mikoa husika wanajitolea katika shughuli hii ambayo ni pamoja na kubainisha walengwa, kuwasajili na kugawa hivi viatu kuanzia wiki hii,na Mikoa iliyochaguliwa imezingatia uhai wa chama na idadi ya voluntia mikoani humo.
Watoto wa shule ya msingi waliokuwepo katika halfa hiyo wakisubiri kuvalishwa viatu hivyo

Baadhi ya wanahabari na wafanyakazi wa msalaba mwekundu wakifuatilia kinachojili

“Vigezo vya kuchaguliwa kwa mikoa hii ni kuwa ni sehemu ambapo  Red Cross inatekeleza huduma za nyumbani (Home Based Care) na miradi mingine.” Alisema  Dr. Nangale.
Red Cross, katika shughuli hii inashirikiana kwa karibu na idara ya ustawi wa jamii na MOHSW; Serikali za mitaa; Wakuu wa shule/vituo; Watendaji wa Kata, wazazi husika, n.k. kuhakikisha watoto wasiojiweza na wasiokuwa na uwezo ndo wananufaika na mpango huu.
Tanzania Red Cross inatoa wito kwa watanzania kwamba, viatu hivi haviuzwi na havitakiwi kuuzwa kwa watoto au wazazi wa watoto.
Mratibu wa mpango huu, Bi. Emma Msuya  amesema kwamba msaada huu wa viatu unatarajiwa kuwa wa miaka mitatu (3), ambapo kila mwaka jozi zipatazo 1,000,000, zitatolewa kwa Tanzania na kampuni hiyo.
Msuya amesema kampuni ya Tom Shoes imesha toa msaada huu wa viatu kwa nchi 43, Tanzania ikiwemo kuanzia mwaka huu wa 2013. Baadhi ya nchi nyingine za kiafrika ambazo zinapata msaada kama huu ni; Kenya, Zambia, Liberia na Malawi.
Tanzania Red Cross inaomba Vyombo vya habari, serikali na wadau wote kusaidia katika kuitaarifu jamii husika  suala zima la mradi huu na kuhakikisha kwamba walengwa wananufaika. Na pia kuhakikisha kwamba hamna mtu anaye ruhusiwa kuuza au kununua aina ya viatu vinavyo gawiwa(Toms Shoes).

Post a Comment

0 Comments