NaBaraka Kizuguto pamoja na Herman kihihwili,IMEWEKWA AGOSTI 27,2013 SAA 10:30 jioni
![]() |
| katibu mkuu wa klabu hiyo Lawrence Mwalusako,akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo |
Klabu ya Yanga
ilipokea barua ya TFF ya tarehe 16/08/2013 kuijulisha adhabu iliyotolewa kwa
Mchezaji Mrisho Ngasa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.
Barua hiyo inataja
adhabu hiyo kuwa nikumfungia Mchezaji Ngasa mechi zipatazo 6 na adhabu ya
kulipa sh. 30milioni pamoja na riba ya asilimia 50% yaani 15milioni na kufanya
jumla ya shilingi 45milioni. Lakini barua hiyo haitaji
kifungu cha Kanuni Yanga
au Ngasa aliyokiuka. ![]() |
| Kutoka kushoto:Mtunza fedha wa Yanga Denis,katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako na Wakili wa Yanga Raymond Wawa |
Yanga inaiona adhabu
hii kuwa ni ya uonevu, kwa Klabu na Mchezaji inayokiuka kanuni za mashindano
hayo, misingi ya sheria na haki za msingi za mlalamikiwa.
Mnamo tarehe
23/8/2013 Klabu ya Yanga Iliwasilisha rufaa yake TFF kupinga adhabu hiyo, na
sababu za rufaa hiyo ni kama ifuatavyo:-
1.
KAMATI ILIKOSEA
KIKANUNI NA KISHERIA KUMWADHIBU NGASA KWA KUZINGATIA MKATABA BATILI
Suala la usajili wa mchezaji Mrisho Ngasa baina yake na Simba Mara
baada ya Msimu wa 2012/2013 kumalizika ulikuwa na matukio makubwa yaliyomhusu
Mchezaji Mrisho Ngasa, Klabu ya Simba na Klabu ya Azam. Kamati ya sheria na
hadhi za wachezaji ya TFF ilipaswa kuyarejea kabla ya kufikia uamuzi waliofikia
hasa kwa kuzingatia mchezaji hakuwepo kujitetea katika kikao hicho.
i.
Tukio baada ya Mechi
kati ya Yanga na Azam Kumalizika katika msimu wa 2012/2013.
Baada ya mechi hiyo
hakuna asiyekumbuka mrisho Ngasa kuonesha mapenzi yake kwa Klabu ya Yanga,
baada ya kuvaa jezi ya yanga na kubebwa na mashabiki wa Yanga.
ii.
Timu ya Azam
Kutangaza kumpeleka Ngasa
Tukio la Ngasa kuvaa
Jezi ya Yanga halikuifurahisha Klabu ya Azam na kutoa mapendekezo ya kumtoa kwa
mkopo kwa klabu iliyokuwa tayari kutoa kiasi cha dola 50,000, na yanga
hawakuafiki kiwango hicho ndipo Simba walifanikiwa kumnyakua Ngasa kwa Mkopo.
Na klabu ya Azam iliutangazia umma wa wa Tanzania kumpeleka Ngasa kwa mkopo
katika klabu ya Simba.Kamati yako pia inaweza kufuatilia katika mtandao wa Azam
fc ( www.azamfc.co.tz).
iii.
Tamko la Mrisho
Ngasa Kushangazwa na uamuzi huo pasipo kushirikishwa.
Baada ya umma
kutangaziwa uamuzi huo Mchezaji Ngasa alitoa tamko kwa umma kupitia vyombo
mbalimbali vya habari Tamko la Ngasa kutokuwa tayari kuuzwa kama mbuzi, kwani
hakushirikishwa. Klabu yake na Simba waliweka msimamo na Ngasa alitishwa kuwa
asingeenda Simba basi angekaa benchi mpaka mwisho wa Mkataba wake.
iv.
Uamuzi wa Klabu ya
Simba Kumkabidhi Ngasa Gari na Pesa.
Baada ya tamko hilo
la Klabu ya Azam na Mchezaji Ngasa. Mchezaji huyo ina semekana alitoweka na
kufunga mawasiliano yake, lakini baadaye alionekana katika vyombo vya habari
vilivyoripoti tarehe 2/8/2012akiwa amepigwa picha akiandika mbele ya Kiongozi
wa Simba. Baada ya sinema hizo Ngasa kwa
unyonge alisikika akisema amekubali kucheza Simba. Na tarehe 3/8/2012 Ngasa
aliripotiwa katika picha na Vyombo vya habari akiwa mbele ya gari iliyosemekana
alipewa na Simba.
v.
Mkakati wa Azam Fc
Kummuza Ngasa Katika Klabu ya Elmerekh
Ikumbukwe pia kuwa
wakati akiwa katika mkataba wa mkopo baina ya simba na Azam, Simba walifanya
utaratibu wa kumumsajili Ngasa, usanii ni mnamo tarehe December 5, 2012 vyombo
vya habari viliripoti Azam yamuuza Ngasa
kwa Elmereikh kwa $ 75,000 sawa na Milioni
120
Suala la kujiuliza
ni kwanini Mkataba waliotia Simba wa tarehe 2/8/2012, haukuizuia Azam kumuuza
Ngasa December 5, 2012? Jibu ni rahisi kwamba Mkataba haukuwa na nguvu yeyote
ya Kikanuni au kisheria kwa maana ya uhamisho na usajili wa wachezaji, ndio
maana Simba hawakupinga, lakini Ngasa alikataa na kujificha hata maafisa wa
timu hiyo walipofika Tanzania bila kuonana na Ngasa.
Katika Mwongozo wa
FIFA juu ya hadhi za wachezaji na masuala ya kinidhamu (FIFA Manual; Players
Status and Disciplinary Matters) kipengele cha 3(d) kinaeleza wazi kuwa katika
kuhakikisha uthibiti wa mkataba baina ya mchezaji na klabu, mahusiano ya
kiajira lazima yazingatie uwiano baina ya matakwa ya mchezaji na ya klabu
(yaani pande zote mbili).
Kifungu cha 3(f) cha
Mwongozo huo unabainisha kuwa kuna vipindi viwili tu vya usajili, katika msimu
mmoja. Swala la kujiuliza Simba waliingia makubaliano na Ngasa katika kipindi
kipi mbali na kuwa katika mkopo kwa msimu mmoja?
Kimsingi Mchezaji
Ngasa hakuwa na mkataba halali na Simba inakuwaje Ngasa awajibishwe kinidhamu
na Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kwa makubaliano ambayo hayatambuliwi
kikanuni na kisheria?
Hata kama imebainika
kuwa Mrisho Ngasa alikuwa na mkataba na klabu ya Simba, ni wazi kuwa katika
maelezo hapo juu hapakuwa na hiari ya mchezaji kuamua kuingia katika mkataba.
Sheria ya Mikataba ya
Tanzaia Sura ya 345 kifungu cha 10 kinatanabaisha kwamba makubaliano yote
yanakuwa mkataba kama yamefanyika kwa hiari na uhuru wa kila upande. Kifungu cha 14 cha sharia hiyo
inaongeza kuwa makubaliano yanakuwa ya hiyari endapo yanafanyika pasipokuwa na
kulazimishwa au shuruti, pasipo kuwa na shinikizo, pasipokuwa na udanganyifu,
au makosa.
Kifungu cha 19 cha
sheria ya mikataba inatanabaisha kuwa pale ambapo hiyari katika mkataba
inapatikana pakiwa na kulazimishwa au hiyari ,shinikizo, udanganyifu au makosa
basi mkataba huo unakuwa ni batilifu ( voidable) kwa upande ambao hiyari
ilipatikana kwa hila hizo hapo katika kifungu cha 19.
Je katika suala hili
endapo Ngasa alipewa fedha na gari kulikuwa na hiyari ya dhati? Ikumbukwe kuwa
Ngasa alitishiwa kuwa asipokubali kucheza Simba angekaa benchi hadi mwisho wa
mkataba wake.
Alikubali kuingia
mkataba akiwa katika upande dhaifu kimaamuzi/weak position, hata mkataba kama
ulikuwepo haukuwa na nguvu kikanuni na kisheria.
2.
KAMATI ILIKOSEA
KIKANUNI NA KISHERIA KUTOA UAMUZI KWA USHAHIDI WA UPANDE MMOJA PASIPO
KUMSIKILIZA MRISHO NGASA.
Ngasa hakupewa
nafasi ya kujitetea juu ya utata wa yanayosemekana makubaliano ya kumpa fedha, Ngasa anaelewa fika alikuwa kwa
mkopo Simba, na kwamba simba hawakuwa na uwezo kwa kanuni za usajili kumpa
mkataba wa usajili kwa wakati huo, suala hilo lingepata majibu mazuri kama
ngasa naye angepewa fursa ya kuelezea alivyouelewa mkataba huo.
Ngasa hakuitwa,
hivyo alinyimwa haki ya msingi ya kusikilizwa. Kamati ilithibitisha vipi tuhuma
za kupokea fedha na kufikia kutoa adhabu kali kama ile ya kurudisha milioni 45
pasipo mtuhumiwa kusikilizwa?
Nakama ilithibitisha
Ngasa kupokea fedha ni kiasi gani? Na kama alipewa gari thamani yake ni kiasi
gani, hivyo vyote huthibitishwa kwa
risiti au bank statement.
Hata Kanunu za
adhabu za FIFA katika kifungu cha kinasisitiza kabla ya kutoa adhabu lazima
mlalamikiwa apewe fursa ya kusikilizwa.
Haya mambo yote
yalipaswa kupatiwa majibu kabla ya kutoa uamuzi na adhabu kwa Yanga na Ngasa,
kwa kutopata maelezo ya Mchezaji, Kamati imemnyima
Ngasa haki ya msingi ya kusikilizwa kabla ya Kuadhibiwa (Aud auteram patem) -the right to be
heard, wala hapakuwa na mtu wa kumtetea.
3.
KAMATI ILIKOSEA
KIKANUNI KUMWADHIBU MCHEZAJI MRISHO NGASA KWA KUINGIA MKATABA NA SIMBA NJE YA
KANUNI ZA USAJILI.
Hakuna shaka Simba
ilimrubuni mchezaji kwa kumshawishi asaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo nje
ya utaratibu wa usajili na bila woga waliuleta mkataba huo na kuweka pingamizi.
Hata kanuni za FIFA
zimeweka adhabu kali kwa viongozi wanao gushi nyaraka za kuweka mahusiano ya
kisheria kama inavyodaiwa na Simba dhidi ya Ngasa, kwa kuwa uhalali wa mkataba
huo unatia mashaka kwa mujibu wa kanuni za usajili na adhabu hutolewa kwa
mujibu wa Chapter II, Section 5 Article
61 ya Kanuni za Adhabu za Fifa (FIFA Disciplinary code) ina tamka wazi kuwa
endapo kutakuwa na udanganyifu au kugushi nyaraka zinazo husiana na shughuli za
mpira ikiwa aliyefanya hayo ni kiongozi adhabu yake ni kufungiwa kwa uchache miezi 12.
Pia endapo Klabu
imekiuka taratibu za usajili kama zilivyowekwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 na 6
vya Kanuni za Hadhi na Uhamisho wa wachezaji za fifa na TFF.
Je endapo alipewa
fedha na gari je ilikuwa ni kwa ajili ya Usajili wa msimu huu au kuridhia
kucheza kwa mkopo akiwa mchezaji wa Azam.
Na kama ilikuwa ni
kwa ajili ya usajili wa Msimu huu kwa nini Azam FC tarehe 5/8/2012 waliamua
kumuuza Ngasa Sudani na bila Simba kuleta malalamiko rasmi TFF?
Je mkataba ulikuwa
ni wa kuichezea Simba kwa msimu huu wa 2013/2014, mkataba huo ulifanyika katika
kipindi mahsusi cha kuingia mkataba na mchezaji au ni makubaliano ya awali
(MOU), kama ni makubaliano ya awali kamati hiyo haikupaswa kujihusisha na makubaliano
hayo. Kwa namna yeyote ile mkatabawa Simba na Ngasa wa tarehe 2/8/2012
ulifanyika ndani ya mkataba wa mkopo na Azam na hivyo mkataba wa Simba ukawa
batili na ndivyo kamati ilivyoona.
Je, kamati ilifanya
sahihi kuutambua mkataba huo pasipo kumuuliza mchezaji na kuamuru kurudisha
fedha na fidia isiyo ya haki wakati kamati haitambui uhalali wa mkataba huo?
Kama vile kamati
iliona haikuwa halali kuiadhibu Simba hivyo hivyo haikuwa na mamlaka kikanuni
kutoa adhabu kwa Ngasa kwa mujibu wa majukumu yaliyo ainishwa katika Kipengele
cha 40(8) cha Katiba ya TFF.
4.
KAMATI ILIKOSEA
KISHERIA KWA WALIOWEKA PINGAMIZI KUWA SEHEMU YA KUTOA UAMUZI
Kamati imekiuka haki ya
msingi inayomzuia mtu kuwa jaji kwenye shauri lake mwenyewe.(“Nemo
Judex in causa sua”)
Kama tulivyoeleza hapo awali, Simba ndio walioweka pingamizi na tuhuma
za mkataba na viongozi wa Simba walikaa katika kamati iliyoamua hatma ya Ngasa
pasipo Ngasa kuwakilishwa kwa vyovyote maamuzi hayangemtendea haki Ngasa.
5.
KAMATI ILIKOSEA
KIKANUNI KUINYIMA KLABU YA YANGA KUMTUMIA NGASA KATIKA MECHI SITA PASIPO NA
SABABU ZA MSINGI.
Kwa kumfungia Ngasa
mechi sita ni kuiadhibu Klabu ya Yanga kwa kosa ambalo kama lipo haijahusika
nalo, Klabu ya yanga imemsajili Ngasa kihalali hivyo kumfungia Ngasa ni uonevu
kwa Yanga.
Haikubaliki
kimantiki kutomruhusu Ngasa kuchezea Yanga wakati huo huo TFF wanamtumia katika
Timu ya taifa, kama ambavyo TFF/Timu ya Taifa haihusiki katika mkataba
batilifu, Yanga nayo haihusiki na makosa yeyote, hivyo ni uonevu kwa Yanga
kutomruhusu Ngasa kuitumikia katika mechi sita.
Ni rai yetu
nyenyekevu Kuomba kamati yako kuifutia Yanga adhabu ya kutomtumia mchezaji
Ngasa katika mechi tano zilizosalia, kwa kuwa katika suala hili Yanga anakuja
mbele ya kamati yako akiwa na mikono safi.


0 Comments