Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA AGOSTI 31,2013 SAA 9:00 USIKU
Penalty ya mwisho aliyokosa Romelu Lukaku imewapa ushindi Bayern Munich katika Europa Super
Cup baada kupigwa penalty
5-4.
Mchuano huo uliokuwa unakumbushia upinzani wa jadi wa makocha wapya wa timu hizo mbili yaani Chelsea na Bayern Munich, kwani Mourihno alikuwa mkufunzi wa Real Madrid huku Guardiola yeye akiwa na Barcelona zote za Uhispania,lakini katika mtanange huo Jose Mourihno(The happy one),aliondoka kichwa chini baada ya penalti ya mwisho.
 |
| Hasara: Lukaku inaonekana kushangaa baada ya kukosa penalty |
|
|
 |
Mabingwa tena: Bayern wanasheherekea ushindi baada ya Lukaku kukosa penalty
|
 |
Kiulaini: Javi Martinez (kulia) akiipatia Bayern bao la pili la kusawazisha katika dakika ya mwisho ya muda wa ziada.
|
Bayern walifanikiwa kutwaa kombe hilo baada ya kumaliza dakika 120 kwa kwenda sare
ya mabao 2-2,ndipo zilipoamuliwa kupingwa penalty na Bayern wakashinda kwa penalty 5 kwa 4 za Chelsea.
Katika mchezo Walioanza kupata bao walikuwa ni Chelsea kupitia kwa
Fernando Torres katika dakika ya 8 ndani ya kipindi cha kwanza,kisha wachezaji wakaenda mapumziko Chelsea wakiwa wanaongoza kwa bao 1 kwa0.Baada ya mapumziko katika dakika ya 47 Franck Ribéry akaisawazishia Bayern,lakini Chelsea walimaliza dakika 90 wakiwa pungufu baada ya Ramires kupewa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 85 baada ya kumchezea vibaya Mario Gotze,na dakika 90 zikawa zimemalizika kwa timu hizo kufungana bao 1 kwa 1.kisha zikaongezwa dakika 30.
Eden Hazard,akiipatia bao la pili Chelsea ndani ya muda wa ziada katika dakika ya 93,na kuifanya timu hiyo kujipa matumaini ya kuondoka na kombe hilo,kwani mpaka dakika 30 za ziada zinakaribia kuisha timu Bayern bado wakiwa hawajasawazisha japo kuwa waliutawala mchezo ndani ya dakika hizo,lakini bayarn walizidi kuzinduka na kuwafanya Chelsea kuzidi kuwa na hofu na hatimaye wakaweza kusawazisha bao la pili kupitia kwa Javier Martinez katika dakika moja ya ziada iliyoongezwa,kwani pia dakika 120 zilikuwa zimeshakwisha.
 |
| Hazard akipachika bao la pili kwa upande wa Chelsea |
 |
Kabla:Hazard akiiwezasha Chelsea kuongoza kwa bao 2-1 katika muda wa ziada
|
 |
| Nenda nje:: Ramires akipewa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 85 baada ya kumchezea vibaya Mario Gotze |
Kisha mwamuzi akaamua Penalty zipigwe,na kwa upande wa Bayern waliopata penalty ni David Alaba,Toni Kroos,Philipp Lahm,Franck Ribéry na Xherdan Shaqir.
Kwa upande wa Chelsea waliopata penarty ni David Luiz,Oscar,Frank Lampard na
Ashley Cole,na aliyekosa alikuwa ni mchezaji kinda aliyetokea kuwa mashuhuri tangu msimu uliopita akiwa kwa
mkopo West Bromwich Albion, Romelu Lukaku ndiye aliyekosa penati na kupeleka
kombe hilo Ujerumani.
 |
| Uwanja ulitapika:mashabiki wa Bayern wakipeperusha bendera kabla ya mchezo |
 |
| Mbwatukaji: Mourinho,hatulii kama kawaida yake |
 |
Asanteeee: Ribery alikwenda moja kwa moja,kwa bosi wa Bayern Pep Guardiola baada ya kufunga bao la kusawazisha
|
 |
| Uwanja mpya:uwanja wa Edeni,ndio uliotumika kwa ajili ya fainali hiyo |
Kikosi cha Bayern Munich: Neuer,
Rafinha (Javi Martinez 56), Dante, Boateng, Alaba, Muller (Gotze 70),
Lahm, Kroos, Ribery, Mandzukic, Robben (Shaqiri 95).
Wachezaji wa akiba: Starke, Van Buyten, Contento, Pizarro.
Kadi ya njano: Ribery
wafungaji: Ribery (47), Javi Martinez (120)
Kikosi cha Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Hazard, Oscar, Schurrle, Torres (Lukaku 97).
Wachezaji wa akiba: Schwarzer, Azpilicueta, Terry, Essien, Mikel, Mata.
Kadi za njano: Cahill, Ramires, Luiz, Torres, Cole, Ivanovic
Kadi nyekundu: Ramires (84)
Wafungaji: Torres (8) Hazard (93)
0 Comments