Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA AGOSTI 30,2013 SAA 2:00 USIKU
Gareth Bale imekubali kufikia makubaliano kuhusiana na maslahi binafsi ya kujiunga na klabu ya Real Madrid,kuelekea usajili
utakaovunja rekodi ya dunia kutoka katika klabu yake ya Tottenham.
utakaovunja rekodi ya dunia kutoka katika klabu yake ya Tottenham.
Hata
hivyo, klabu ya Real madridi bado iko katika majadiliano juu ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 , kwa jitihada za fedha ya £ 86m ambayo tayari imewasilishwa
kwa Spurs.
Mwandishi mkuu wa habari za michezo kutoka shirika la habari la BBC Dan Roan,amesema Makubaliano juu ya suala binafsi,hakuna kizuizi juu ya hilo, na wakati mazungumzo yaliyochukuwa siku kazaa na Madrid,kulikuwa hakuna kikwazo kuhusiana na swala hilo.
![]() |
| Cristiano Ronaldo:Rekodi yake inatarajiwa kuvunjwa |
Iwapo Spurs watakubali rasmi ofa hiyo ya Real Madrid ,basi ofa hiyo itakuwa ni ya rekodi ya dunia,na kuishinda ile waliyopewa Manchester United ya £ 80m mwaka 2009 kwa Cristiano Ronaldo kwenda Real Madrid.


0 Comments