Ticker

6/recent/ticker-posts

IKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUKUKUTANA NA RHINO RANGERS HAPO KESHO KATIKA MECHI YAO YA UFUNGUZI WA LIGI KUU,SIMBA YA KAMATA MZIGO

na Herman Kihwili IMEWEKWA AGOSTI 23,2013 SAA 12:00 jioni
Timu ya mchezo wa soka ya Simba ya jijini dar es salaam,imenzisha rasmi mchakato wa kukamata jezi feki zilizo zagaa mtaani,ili kuweza kulinda haki miliki za klabu hiyo.
Masoud Said Masoud Msimamizi wa zoezi  la kamatakaata,akitoa ufafanuzi juu ya jezi feki
Akizungumaza na Jamii na Michezo Msimamizi wa zoezi hilo la
kamatakaata,Masoud Said Masoud amesema zoezi hilo ni endelevu,na kuwataka mashabiki wa klabu hiyo  kuwa makini na jezi hizo, kwa  sababu jezi nyingi zilizozagaa mtaani hazina nembo halali ya klabu hiyo.
Lundo la jezi feki za simba zilizokamatwa leo.
Katika siku hii ya leo Jamii na Michezo imeshuhudia Shehena ya lundo la jezi feki zilizokamatwa na polisi kwa kushilikiana na kampuni ya Isere Sport Company iliyopewa ruksa ya kuendesha zoezi hilo.

Katika hatua nyingine timu hiyo ya wekundu wa Msimbazi,kesho inatupa karata yake ya kwanza katika mchezo wao wa kwanza katika msimu mpya wa 2013/2014 wa ligi kuu,ambapo watakutana na Rhino Rangers,mchezo unaotarajiwa kupigwa   katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
ofisa habari wa timu ya simba,Ezekiel Kamwaga,alipokuwa anazungumza hii leo
Akizungumza na Jamii na Michezo ofisa habari wa timu ya simba,Ezekiel Kamwaga,amesema wanaingia katika mchezo huo wakiwa wamekamilika sekta zote,na wanamuamini kocha wao Abdallah King Kibaden Mputa alivyowanoa vijana wake,na pia wana uhakika wa kufanya vizuri katika msimu huu,kwa kuwa wamefanya usajili mzuri kwa kuziba mapengo yote muhimu ikiwemo nafasi ya ushambuliaji.
mashabiki wa simba wakiwa makao makuu ya klabu hiyo ya simba,wakijianda kueleke Tabora mapema leo hii.
Pia klabu hiyo ya simba,imewataka marefa kuchezesha mpira kwa haki na kuzingatia sheria 17 za mchezo,kwani kwenda kinyume na hapo,refa atakuwa unajishushia samani yeye mwenyewe kwani atakuwa anatazamwa na viongozi mbalimbali wa mchezo wa soka duniani,na pia anaweza kujikosesha nafasi mbalimbali za kuchezesha mpira kokote duniani.



Post a Comment

0 Comments