Ticker

6/recent/ticker-posts

HAPA NDIPO MAISHA YA WASANII YATAKAPO KUWA


Na.John Peter,iMEWEKWA AGOSTI 28,2013 SAA 7:00 mchana
Hii ni nyumba ambayo imekamilika
Naibu waziri wa kilimo na chakula Mh.Adam Malima anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  siku ya jumamosi ya tarehe 31 agost 2013 katika sherehe ya kuwakabidhi nyumba baadhi ya wasanii wa Tanzania
katika kijiji cha wasanii kilichopo wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Hii ni  moja ya nyumba ambayo inaendelea kujengwa
Akiongea na Jamii na Michezo mwenyekiti wa shilikisho la mtandao wa wasanii[ shiwata]Cassim Taalib amesema kuwa ujenzi wa baadhi ya nyumba umekamilika na siku hiyo wasanii ambao wamekamilisha kujenga watakabidhiwa hati za nyumba zao na mgeni rasmi ambaye ni naibu waziri wa kilimo na chakula,pia ni mbunge wa jimbo la Mkuranga,.ADAM MALIMA.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiingia ndani ya nyumba ya kijiji cha wasanii
Taalib amesema kuwa kijiji hicho cha wasanii kina ukubwa wa ekari mia tatu [300]pia kipo umbali wa kilomita kumi kutoka Mkuranga mjini.kijiji hicho ambacho kimetengwa kwa ajili ya wasanii pamoja na waandishi wa habari  pia Taalib ametoa wito kwa wasanii kuungana ili kuwezesha kijiji hicho kusonga mbele

Tayari mpaka sasa nyumba kumi na moja za tofari zimejengwa na mabanda zaidi ya thalathini nayo yamejengwa

Post a Comment

0 Comments