Mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi
Simba leo wamewasili kisiwani Unguja, tayari kwa michuano ya Mapinduzi Cup
iliyoanza
rasmi jana kwenye uwanja wa Aman.
Simba imewasili visiwani humo majira ya saa tano
asubuhi ikiwa na kikosi chake kamili, iliongozwa na kocha mkuu Patrick Aussems
ambaye alizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha taratibu za
bandarini.
Kocha Aussems amesema michuano ya kombe la Mapinduzi
ni njia sahihi kwake kuandaa timu kuelekea mchezo wao wa kwanza wa hatua ya
makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambao utachezwa mwishoni
mwa juma lijalo jijini Dar es salaam, dhidi ya Js Saouro ya Algeria.
Bofya kusikiliza
0 Comments