Kampuni ya kubashiri matokeo ya michezo ya Sports Pesa inaendelea
kukamilisha maandalizi ya
michuano yua Sports Pesa Super Cup
itakayofanyika nchini Tanzania kuanzia February 22.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji SportPesa Tanzania Tarimba Abbas
amesema tayari wameshakamilisha utaratibu wa kuzialika timu shiriki kwa
mwaka huu 2018, huku wakiamini timu za tanznaia zitakua na kila sababu
ya kutorejea makosa waliyoyafanya miaka miwiwli iliyopita kwa kuuacha
ubingwa kuchukuliwa na Gor Mahia ya nchini Kenya.
Tarimba amesema michuano ya Sports Pesa Super Cup kwa mwaka huu pia
itatumika kwa ajili ya kuwaandaa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC
ambao mwanzoni mwa mwezi Februari watakua na kibarua cha kuikabili Al
Ahly kutoka Misri.
Bofya Chini Kutazama
0 Comments