Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA 10,SEPT.2018 SAA 03:17 USIKU
..>>>..
Shirikisho la soka nchini TFF limewakumbusha
wanachama wake juu ya mpango wa kuzialika timu kutoka nje ya nchi kwa ajili ya
kucheza michezo ya
kirafiki ama kushiriki michuano ya soka.
TFF wamewakumbusha wnaachama wake suala hilo, kufuatia
ujio wa klabu ya AFC Leopard kutoka nchini Kenya iliyocheza na Simba mwishoni
mwa juma lililopita jijini Dar es salaam, kuwa na ukakasi.
Mualiko mwingine ambao ulikua na ukakasi ni ile
ulioihusisha klabu ya Sonny Sugar ambayo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya
Biashara United mkoani Mara.
Mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho hilo Salum
Madadi amesema kuna ulazima kwa wanachama wa TFF wakajikumbusha utaratibu
uliopo kisheria wa kuzialika timu kutoka nje ya nchi na kucheza michezo wa
kirafiki ya kimataifa, ili kutambua nafasi zao chini ya mwamvuli wa mamlaka ya
soka nchini.
Bofya chini Kusikiliza
0 Comments