Ticker

6/recent/ticker-posts

Unamruhusu Okwi Ili atumalize,Kisha Bocco unamkataza-Tff baada ya kumfungia meneja wa Simba Sc

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA 10,SEPT.2018 SAA 02:37 USIKU
Sakata la wachezaji wa klabu ya SImba kushindwa kufika kwa wakati kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na kupelekea kuondolewa kwenye kikosi na kocha mkuu
Emmanuel Amunike majuma mawili yaliyopita, limemalizwa rasmi kwa meneja wa klabu hiyo Robert Richard kufungiwa kujihusisha na soka kwa muda wa mwaka mmoja.

Adhabu kwa kiongozi huyo ambaye ni sehemu ya benchi la ufundi, imetolewa na kamati ya madili ya shirikisho la soka nchini, ambayo ilifikishiwa malalamiko ya kimaadili na sekretarieti ya shirikisho hilo inayoongozwa na katibu mkuu Wilfred Kidau.

Hamidu Mbwezeleni

 Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya TFF Hamidu Mbwezeleni mapema hii leo alizungumza na waandishi wa habari na kutangaza hukumu ya kifungo kwa meneja wa klabu ya Simba, baada ya kamati yake kukutana katika vikao vitatu.

 Kabla ya kutangaza hukumu hiyo mwenyekiti Mbwezeleni alieleza kwa kina sakata hilo lilipoanzia kwa mujibuw a kesi iliyokua mbele yao hadi walipobaini meneja wa Simba ana kila sababu za kuadhibiwa kwa makosa ya kuihujumu timu ya taifa, huku jija la kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Khamis Kisiwa likitajwa.
ANGALIA VIDEO

..

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo),na instagram- kihwiliupdates

Post a Comment

0 Comments